081 - At-Takwiyr

 

 

 

التَّكْوِير

At-Takwiyr: 081

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

إِذَا الشَّمْسُ كُوِّرَتْ ﴿١﴾

1. Jua litakapokunjwa kunjwa na kupotea mwanga wake.

 

 

وَإِذَا النُّجُومُ انكَدَرَتْ ﴿٢﴾

2. Na nyota zitakapoanguka, kupuputika na kutawanyika. 

 

 

وَإِذَا الْجِبَالُ سُيِّرَتْ ﴿٣﴾

3. Na milima itakapoendeshwa iondoke ilipo.

 

 

وَإِذَا الْعِشَارُ عُطِّلَتْ ﴿٤﴾

 

4. Na ngamia wenye mimba pevu watakapotelekezwa.

 

 

وَإِذَا الْوُحُوشُ حُشِرَتْ ﴿٥﴾

5. Na wanyama mwitu watakapokusanywa.

 

 

وَإِذَا الْبِحَارُ سُجِّرَتْ ﴿٦﴾

6. Na bahari zitakapojazwa na kuwashwa moto.

 

 

وَإِذَا النُّفُوسُ زُوِّجَتْ ﴿٧﴾

7. Na nafsi zitakapounganishwa na roho kisha kwa aina zake (wema kwa wema, waovu kwa waovu).

 

 

وَإِذَا الْمَوْءُودَةُ سُئِلَتْ ﴿٨﴾

8. Na mtoto wa kike aliyezikwa akiwa yuhai atakapoulizwa.

 

 

بِأَيِّ ذَنبٍ قُتِلَتْ ﴿٩﴾

9. Kwa dhambi gani aliuliwa?

 

 

وَإِذَا الصُّحُفُ نُشِرَتْ ﴿١٠﴾

10. Na sahifa za kurekodi (amali) zitakapotandazwa (na kukunjuliwa).

 

 

وَإِذَا السَّمَاءُ كُشِطَتْ ﴿١١﴾

11. Na mbingu zitakapobanduliwa.

 

 

وَإِذَا الْجَحِيمُ سُعِّرَتْ ﴿١٢﴾

12. Na moto uwakao vikali mno utakapowashwa.

 

 

وَإِذَا الْجَنَّةُ أُزْلِفَتْ ﴿١٣﴾

13. Na Jannah itakapoletwa karibu.

 

 

عَلِمَتْ نَفْسٌ مَّا أَحْضَرَتْ ﴿١٤﴾

14. Nafsi itajua hapo yale iliyoyahudhurisha.

 

 

فَلَا أُقْسِمُ بِالْخُنَّسِ ﴿١٥﴾

15. Basi Naapa kwa sayari zinazotoweka (mchana na zinadhihirika usiku).

 

 

الْجَوَارِ الْكُنَّسِ ﴿١٦﴾

16. Zinazotembea na kujificha.

 

 

وَاللَّيْلِ إِذَا عَسْعَسَ ﴿١٧﴾

17. Na Naapa kwa usiku unapoingia. 

 

 

وَالصُّبْحِ إِذَا تَنَفَّسَ ﴿١٨﴾

18. Na Naapa kwa asubuhi inapopambazuka.

 

 

إِنَّهُ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ ﴿١٩﴾

19. Hakika hii (Qur-aan) bila shaka ni kauli ya Mjumbe Mtukufu (Jibriyl).

 

 

ذِي قُوَّةٍ عِندَ ذِي الْعَرْشِ مَكِينٍ ﴿٢٠﴾

20. Mwenye nguvu na cheo kitukufu kwa (Allaah) Anayemiliki ‘Arsh.

 

 

مُّطَاعٍ ثَمَّ أَمِينٍ ﴿٢١﴾

21. Anayetiiwa (na Malaika), mwaminifu huko (mbinguni).

 

 

 

وَمَا صَاحِبُكُم بِمَجْنُونٍ ﴿٢٢﴾

22. Na hakuwa swahibu yenu (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) majnuni.

 

 

وَلَقَدْ رَآهُ بِالْأُفُقِ الْمُبِينِ ﴿٢٣﴾

23. Na kwa yakini alimuona (Jibriyl) katika upeo wa macho ulio bayana.

 

 

وَمَا هُوَ عَلَى الْغَيْبِ بِضَنِينٍ ﴿٢٤﴾

24. Naye si mzuiaji wa (kuelezea mambo ya) ghaibu.

 

 

وَمَا هُوَ بِقَوْلِ شَيْطَانٍ رَّجِيمٍ ﴿٢٥﴾

25. Na hii (Qur-aan) si kauli ya shaytwaan aliyetokomezwa mbali na kulaaniwa.

 

 

فَأَيْنَ تَذْهَبُونَ ﴿٢٦﴾

26. Basi mnakwenda wapi?

 

 

إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَالَمِينَ ﴿٢٧﴾

27. Hii (Qur-aan) si chochote isipokuwa ni ukumbusho kwa walimwengu.

 

 

لِمَن شَاءَ مِنكُمْ أَن يَسْتَقِيمَ ﴿٢٨﴾

28. Kwa yule atakaye miongoni mwenu anyooke (katika haki)

 

 

وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ ﴿٢٩﴾

29. Na hamtotaka isipokuwa Atake Allaah Rabb wa walimwengu.

 

 

Share