086 - Atw-Twaariq

 

الطَّارِق

 

086-At-Twaariq

 

086-Atw-Twaariq: Utangulizi Wa Suwrah

 

Alhidaaya.com

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

وَالسَّمَاءِ وَالطَّارِقِ ﴿١﴾

1. Naapa kwa mbingu na kinachogonga kinapotoka usiku[1].

 

 

وَمَا أَدْرَاكَ مَا الطَّارِقُ ﴿٢﴾

2. Na kipi kitakachokujulisha kinachogonga na kutoka usiku?

 

 

النَّجْمُ الثَّاقِبُ ﴿٣﴾

3.  Ni nyota yenye mwanga mkali mno inayopenya kwa nguvu.  

 

 

إِن كُلُّ نَفْسٍ لَّمَّا عَلَيْهَا حَافِظٌ ﴿٤﴾

4. Hakuna nafsi yeyote isipokuwa inayo mhifadhi juu yake. 

 

 

فَلْيَنظُرِ الْإِنسَانُ مِمَّ خُلِقَ ﴿٥﴾

5. Basi na atazame binaadamu ameumbwa kutokana na kitu gani?

 

 

خُلِقَ مِن مَّاءٍ دَافِقٍ ﴿٦﴾

6. Ameumbwa kutokana na maji yatokayo kwa mchupo.

 

 

يَخْرُجُ مِن بَيْنِ الصُّلْبِ وَالتَّرَائِبِ ﴿٧﴾

7. Yanatoka baina ya uti wa mgongo na mbavu za kifua.

 

 

إِنَّهُ عَلَىٰ رَجْعِهِ لَقَادِرٌ ﴿٨﴾

8. Hakika Yeye (Allaah) bila shaka Ni Muweza[2] wa Kumrudisha (hai).

 

 

يَوْمَ تُبْلَى السَّرَائِرُ ﴿٩﴾

9. Siku siri zitakapopekuliwa (na kufichuka).

 

 

فَمَا لَهُ مِن قُوَّةٍ وَلَا نَاصِرٍ ﴿١٠﴾

10. Basi hatakuwa na nguvu yoyote wala mwenye kunusuru yeyote.

 

 

وَالسَّمَاءِ ذَاتِ الرَّجْعِ ﴿١١﴾

11. Naapa kwa mbingu yenye marejeo (ya kuleta mvua).

 

 

وَالْأَرْضِ ذَاتِ الصَّدْعِ ﴿١٢﴾

12. Na Naapa kwa ardhi yenye kupasuka (kutoa mimea).

 

 

إِنَّهُ لَقَوْلٌ فَصْلٌ ﴿١٣﴾

13. Hakika hii (Qur-aan) ni kauli pambanushi (kati ya haki na baatwil).

 

 

وَمَا هُوَ بِالْهَزْلِ ﴿١٤﴾

14. Nayo si mzaha.

 

 

إِنَّهُمْ يَكِيدُونَ كَيْدًا ﴿١٥﴾

15. Hakika wao wanapanga hila.

 

 

 

وَأَكِيدُ كَيْدًا ﴿١٦﴾

16. Nami Natibua hila (zao).

 

 

فَمَهِّلِ الْكَافِرِينَ أَمْهِلْهُمْ رُوَيْدًا ﴿١٧﴾

17. Basi wape makafiri muhula, wape muhula taratibu.

 

 

 
Share