092 - Al-Layl

 

 

 

  اللَّيْل

Al-Layl: 092

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

وَاللَّيْلِ إِذَا يَغْشَىٰ ﴿١﴾

1. Naapa kwa usiku unapofunika.

 

 

وَالنَّهَارِ إِذَا تَجَلَّىٰ ﴿٢﴾

2. Na Naapa kwa mchana unapodhihirika mwanga wake.

 

 

وَمَا خَلَقَ الذَّكَرَ وَالْأُنثَىٰ ﴿٣﴾

3. Na Naapa kwa Aliyeumba dume na jike.

 

 

إِنَّ سَعْيَكُمْ لَشَتَّىٰ ﴿٤﴾

4. Hakika juhudi zenu bila shaka ni tofauti tofauti.

 

 

فَأَمَّا مَنْ أَعْطَىٰ وَاتَّقَىٰ ﴿٥﴾

5. Basi yule anayetoa (mali) na akamcha Allaah.

 

 

وَصَدَّقَ بِالْحُسْنَىٰ ﴿٦﴾

6. Na akasadikisha Al-Husnaa (Jazaa na Kalimah ya laa ilaaha illa Allaah). 

 

 

فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْيُسْرَىٰ ﴿٧﴾

7. Basi Tutamuwepesishia kwa yaliyo mepesi.  

 

 

وَأَمَّا مَن بَخِلَ وَاسْتَغْنَىٰ ﴿٨﴾

8. Ama yule afanyaye ubakhili na akajiona amejitosheleza.

 

 

وَكَذَّبَ بِالْحُسْنَىٰ ﴿٩﴾

9. Na akakadhibisha Al-Husnaa (Jazaa na Kalimah ya laa ilaaha illa Allaah). 

 

 

فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْعُسْرَىٰ ﴿١٠﴾

10. Basi Tutamuwepesishia kwa yaliyo magumu.

 

 

وَمَا يُغْنِي عَنْهُ مَالُهُ إِذَا تَرَدَّىٰ ﴿١١﴾

11. Na itamsaidia nini mali yake atakapoporomoka kuangamia (motoni)?!

 

 

 

 

إِنَّ عَلَيْنَا لَلْـهُدَىٰ ﴿١٢﴾

12. Hakika ni juu Yetu (kubainisha) mwongozo.

 

 

وَإِنَّ لَنَا لَلْآخِرَةَ وَالْأُولَىٰ ﴿١٣﴾

13. Na hakika ni Yetu Sisi Aakhirah na awali (dunia).

 

 

فَأَنذَرْتُكُمْ نَارًا تَلَظَّىٰ ﴿١٤﴾

14. Basi Nimekutahadharisheni moto wenye mwako mkali mno.

 

 

لَا يَصْلَاهَا إِلَّا الْأَشْقَى ﴿١٥﴾

15. Hatouingia kuungua isipokuwa muovu mkubwa.

 

 

الَّذِي كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ ﴿١٦﴾

16. Ambaye amekadhibisha na akakengeuka mbali.

 

 

وَسَيُجَنَّبُهَا الْأَتْقَى ﴿١٧﴾

17. Na ataepushwa nao mwenye taqwa imara zaidi.

 

 

الَّذِي يُؤْتِي مَالَهُ يَتَزَكَّىٰ ﴿١٨﴾

18. Ambaye anatoa mali yake kujitakasa.

 

 

وَمَا لِأَحَدٍ عِندَهُ مِن نِّعْمَةٍ تُجْزَىٰ ﴿١٩﴾

19. Na hali hakuna mmoja yeyote aliyemfanyia fadhila yoyote hata amlipe.

 

 

إِلَّا ابْتِغَاءَ وَجْهِ رَبِّهِ الْأَعْلَىٰ ﴿٢٠﴾

20. Isipokuwa kutaka Wajihi wa Rabb wake Mwenye ‘Uluwa Aliyetukuka kabisa kuliko vyote.

 

 

وَلَسَوْفَ يَرْضَىٰ ﴿٢١﴾

21. Na bila shaka atakuja kuridhika.

 

Share