Ukimbizi Na Kubadilisha Jina La Baba
SWALI:
Assalam alaykum
Napenda kuuliza suali. Mimi naishi
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho
Kulingana na mafunzo ya Kiislamu kudanganya ni haramu, Kubadilisha uraia hakuna ubaya lakini kusiwe kinyume cha Sheria ya Kiislamu kwa mfano; kwa njia ya udanganyifu na kadhalika.
Ile nchi uliotoka ikiwa unafanya hijra (kuhama) kwa sababu ya kudhulumiwa kwa ibada au haki nyiginezo uhame kwenda nchi ambayo utapata uhuru wa kuendesha ibada zako bila pingamizi zozote, kupata hali ya kimaisha bora, na kadhalika. Lakini kuhama huku kusiwe kwa gharama ya dini yako.
Asli katika Uislamu, Hijra ni kuhama kutoka nchi ya kikafiri kwenda katika nchi ya Kiislamu au ya Waislamu. Mtu kubadalisha jina la babake haifai, Allaah سبحانه وتعالى Amesema:
}}ادْعُوهُمْ لِآبَائِهِمْ هُوَ أَقْسَطُ عِندَ اللَّهِ{{
{{Waiteni kwa (majina ya) baba zao, maana huo ndio uadilifu mbele ya Mwenyezi Mungu}}
Ahzaab 33:5
Wa Allaahu A'alam
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


