Samaki Wa Kupaka Tui La Nazi La Bizari Ya Mchuzi

 

Samaki Wa Kupaka Tui La Nazi

  

Vipimo

Samaki mkubwa - 1

Tui la nazi zito - 1 gilasi

Pilipili mbichi zilosagwa - 7 kiasi

Chumvi - Kiasi

Ndimu - 2 kamua

Bizari mchuzi - 1 kijiko cha chai 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika  

  1. Msafishe samaki mweke achuje maji
  2. Katika kibakuli kidogo, weka pilipili mbichi, chumvi na ndimu, igawe kiasi kidogo bakisha kando
  3. Mpake samaki kwa mchanganyiko wa pilipili akolee nje na ndani kisha mwache samaki katika friji muda kiasi nusu saa au zaidi yake.
  4. Paka mafuta kidogo treya ya samaki, mweke samaki kisha mchome kwa moto wa juu katika oveni (Grill)
  5. Akiwiva upande mmoja mgeuze kisha mwepue na umweke katika sahani ya kupakulia.
  6. Katika sufuria ndogo, weka tui la nazi mchanganyiko wa pilipili na bizari mchuzi, wacha ichemke kidogo tu huku ukikoroga kwa moto mdogo kiasi cha dakika moja
  7. Paka tui hilo juu ya samaki akiwa tayari

 

 

Share