Kunyoa Nywele Zilizokuwa Hazikutajwa Katika Sunnah Kama Nywele Za Kifuani

 

SWALI

ASSALAMU ALAYKUM.
Kwanza awali ya yote napenda kuwapa pongezi kwa kutujibu masuala ya ndugu zako kwenye Uislamu. Mimi kwa leo napenda kujua hukumu ya kunyoa nywele zilizokuwa hazijanasibishwa na sunna ya Mtume Muhammad (SAW). Kwa mfano, mimi nina nywele nyingi za kifuani na huwa zinaniletea kero kama joto jingi na pia huweka uchafu mwingi ilhali huwa najisafisha sana tu, lakini bado uchafu hautoki. Sasa kama Sunna inasema uislamu ni usafi, kwa nini tuzuiwe japo kuzipunguza nywele kama hizi? Maana nnavyojuwa kuwa hata nywele za kichwani usipozipunguza basi uchafu utajikusanya. Napenda kujua hukmu ya hili. Ahsante.



JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani kwa kaka yetu kuhusu swali hili. Uhakika ni kuwa Uislamu umejengewa katika unadhafa wa kimwili, mavazi, sehemu anayoishi mtu na sehemu nyenginezo. Katika huu unadhafa ni kuchukua udhu, kuoga na kufanya mengineyo kama kukata nywele za kinena, za makapwa, kupunguza masharubu lakini kuacha ndevu. Imechukuliwa kuwa nywele za kifua zitakuwa nyingi na utakuwa huwezi kuweka usafi unaohitajika basi unaweza kunyoa kwani hakuna nasw ya kukataza.

Na Allah Anajua zaidi.

 

Share