271-Aayah Na Mafunzo: Anayetoa Swadaqah Kwa Kuficha Atakuwa Chini Ya Kivuli Cha Allaah

 

 

Al-Baqarah

Anayetoa Swadaqah Kwa Kuficha Atakuwa Chini Ya Kivuli Cha Allaah

 www.alhidaaya.com

 

إِن تُبْدُوا الصَّدَقَاتِ فَنِعِمَّا هِيَ ۖ وَإِن تُخْفُوهَا وَتُؤْتُوهَا الْفُقَرَاءَ فَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۚ وَيُكَفِّرُ عَنكُم مِّن سَيِّئَاتِكُمْ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿٢٧١﴾

 271. Mkidhihirisha swadaqah basi ni vizuri hivyo, na mkizificha na kuwapa mafakiri, basi hilo ni kheri kwenu. Na Atakufutieni katika maovu yenu. Na Allaah kwa yale myatendayo ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika

 

 

Mafunzo:

 

Thawabu za kuficha ‘amali ya kutoa kwa ajili ya Allaah; Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:  “Watu saba ambao Allaah (تعالى) Atawafunika katika kivuli Chake, Siku ambayo hakutokuwa na kivuli ila kivuli Chake; Imaam (kiongozi) muadilifu, kijana ambaye amekulia katika ‘ibaadah ya Rabb wake, mwanamume ambaye moyo wake umegandana (au umeambatana) katika Masjid. Watu wawili wanaopendana kwa ajili ya Allaah wanakutana kwa ajili Yake na wanafarikiana kwa ajili Yake, na mwanamume aliyetakwa na mwanamke mrembo akasema: Mimi namkhofu Allaah, na mwanamume aliyetoa swadaqah yake akaificha hata mkono wa kushoto usijue nini ulichotoa mkono wa kulia, na mwanamume aliyemdhukuru Allaah pekee macho yake yakatokwa machozi.” [Al-Bukhaariy na Muslim] 

 

 

Share