Skip to main content

Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)073-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Maghfirah Kwa Makosa Uliyoyakusudia Na Ya Mzaha, Kinga Ya Kupinduka Mipaka...

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

Kuomba Maghfirah Kwa Makosa Uliyoyakusudia Na Ya Mzaha,

Kuomba Kinga Ya Ujahili Na Kupinduka Mipaka

 Alhidaaya.com

 اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي خَطِيئَتِي وَجَهْلِي وَإِسْرَافِي فِي أمْرِي وَمَا أنْتَ أعْلَمُ بِهِ مِنِّي، اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي جِدِّي وَهَزْلِي وَخَطَئِي وَعَمْدِي وَكُلُّ ذَلِكَ عِنْدِي. اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي مَا قَدَّمْتُ وَمَا أخَّرْتُ وَمَا أسْرَرْتُ وَمَا أعْلَنْتُ وَمَا أنْتَ أعْلَمُ بِهِ مِنِّي، أنْتَ الْمُقَدِّمُ وَأنْتَ الْمُؤَخِّرُ وَأنْتَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ

Allaahumma-ghfirliy khatwiy-atiy, wajahliy, waisraafiy fiy amriy, wamaa Anta A’lamu minniy. Allaahumma-ghfirliy jaddiy, wahazliy, wakhatwa-iy, wa-‘amdiy wa kullu dhaalika ‘indiy. Allaahumma-ghfirliy maa qaddamtu, wamaa akhkhartu, wamaa asrartu, wamaa a’lantu, wamaa Anta A’lamu bihi minniy, Antal-Muqaddimu wa-Antal-Muakhkhiru, wa-Anta ‘alaa kulli shay’in Qadiyr

Ee Allaah! Nighufurie makosa yangu, ujahili (ujinga) wangu, na israaf (upindukaji mipaka) katika mambo yangu, Unayoyajua Wewe kutoka kwangu. Ee Allaah! Nighufurie niliyoyafanya kwa kudhamiria, na niliyoyafanya kwa kukosea, na makosa yangu yote. Ee Allaah! Nighufurie niliyoyatanguliza na niliyoyachelewesha, na niliyoyaficha, na niliyoyadhihirisha, na ambayo Wewe Unayajua kuliko mimi, Wewe ni Mwenye kutanguliza, na Wewe ni mwenye kuchelewesha. Wewe ni Muweza juu ya kila kitu. 

[Al-Bukhaariy, Muslim]