Vikeki Vya Vikombe Vya Raspberry Vya Smarties

Vikeki Vya Vikombe Vya Raspberry Vya Smarties

 

 

Vipimo

 

Unga mweupe vikombe  2 ½   

Siagi kikombe 1 iliyoyayuka

Sukari kikombe 1

Mayai 6

Maziwa ½ kikombe

Baking powder vijiko 2 vya chai

Arki ya Raspberry 1 kijiko cha chai (Raspberry flavour)

Rangi nyekundu ¼ kijiko cha chai

Smarties kiasi

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Washa oveni moto wa kiasi cha 300 – 350 Deg F
  2. Saga sukari na siagi mpaka iwe laini.
  3. Tia mayai na kuchanganya, tia arki ya raspberry  na rangi. Tia maziwa changanya.  
  4. Changanya unga baking powder kisha mimina kidogo kidogo umimine katika vikaratasi vya keki usijae tia ifikiei ¾ ya kikombe cha karatasi.
  5. Nyunyizia smarties.

  1. Tia katika oven pike  (Bake) kiasi nusu saa mpaka iwive.
  2. Epua ipoe katakata ikiwa tayari.

 Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)  

 

 

Share