11-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah: Atakayekiri Na Kushuhudia Laa Ilaaha Illa Allaah Akiyasadikisha Moyoni Ataharamishwa Na Moto.

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah

 

www.alhidaaya.com

 

11-Atakayekiri Na Kushuhudia Laa Ilaaha Illa Allaah Akiyasadikisha Moyoni Ataharamishwa Na Moto.

 

 

عَنْ أنَس بِن مالِك رضي الله عنه عن النَّبِيّ صلى الله عليه وسلم قال: (( مَا مِنْ أَحَدٍ يَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ ، وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللَّهِ صِدْقًا مِنْ قَلْبِهِ إِلَّا حَرَّمَهُ اللَّهُ عَلَى النَّارِ))

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakuna mtu atakayekiri na kushuhudia kwa kusadikisha moyoni mwake kwamba: laa ilaaha illa Allaah – hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, na kwamba Muhammad ni Rasuli wa Allaah, isipokuwa Allaah Atamharamisha na Moto)). [Al-Bukhaariy (128) Muslim (32)]

 

 

Share