22-Fadhila Za Laa ilaaha Illa-Allaah: Thawabu Za Kuacha Huru Watumwa Kumi Kuandikiwa Mema Mia Kufutiwa Maovu Mia Ni Kinga Ya Shaytwaan Na Atakuwa Mtu Bora Kabisa

 

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah

 

22-Thawabu Za Kuacha Huru Watumwa Kumi,

Kuandikiwa Mema Mia, Kufutiwa Maovu Mia,

Ni Kinga Ya Shaytwaan Kwa Siku Hiyo,

Na Hatakuwa Mtu Yeyote Mbora Kumshinda Ila Yule Aliyefanya Zaidi Yake

www.alhidaaya.com

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ : ((مَنْ قَالَ : لاَ إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ، لَهُ المُلْكُ وَلَهُ الحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ، فِي يَوْمٍ مِائَةَ مَرَّةٍ ، كَانَتْ لَهُ عَدْلَ عَشْرِ رِقَابٍ ، وَكُتِبَتْ لَهُ مِائَةُ حَسَنَةٍ ، وَمُحِيَتْ عَنْهُ مِائَةُ سَيِّئَةٍ، وَكَانَتْ لَهُ حِرْزًا مِنَ الشَّيْطَانِ يَوْمَهُ ذَلِكَ حَتَّى يُمْسِيَ ، وَلَمْ يَأْتِ أَحَدٌ بِأَفْضَلَ مِمَّا جَاءَ بِهِ ، إِلَّا أَحَدٌ عَمِلَ أَكْثَرَ مِنْ ذَلِكَ)) البخاري  ومسلم

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Atakayesema kwa siku mara mia,

 

لا إلهَ إلاّ اللّهُ وحْـدَهُ لا شَـريكَ لهُ، لهُ المُـلْكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كُلّ شَيءٍ قَدير

Laa ilaaha illa-Allaahu Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku walahul-Hamdu wa Huwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyr.  

 

Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah  Peke Yake, Hana mshirika, ni Wake Ufalme, na ni Zake Himdi na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza, basi atapata sawa na thawabu za kuwaacha huru watumwa kumi na ataandikiwa mema mia moja na atafutiwa maovu mia moja, na atakuwa na kinga ya shaytwaan kwa siku hiyo yote hadi jioni na hatakuwa mtu yeyote mbora kumshinda ila yule aliyefanya zaidi yake)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

Share