Rock-cakes Za Njugu Na Matunda Makavu

Rock-cakes Za Njugu Na Matunda Makavu 

 

 

VIPIMO:

 

Unga - 4 Vikombe

Sukari -10 Ounce

Siagi - 10 Ounce

Mdalasini ya unga - 2 vijiko vya chai

Matunda makavu/njugu (kama lozi, Zabibu, maganda ya chungwa, Cherries na kadhalika -  4 ounce

Maziwa ya maji  -   4 Vijiko vya supu

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

  1. Chukua siagi na sukari koroga na mixer mpaka iwe kama cream.
  2. Tia vanilla mdalasini, tia yai moja mix tena endelea kuongeza yai lingine mpaka umalize yote, changanya mpaka iwe laini kama sufi (fluffy)
  3. Tia unga na baking powder na dried fruits, changanya na mwiko.
  4. Chota mchanganyiko  na kijiko cha soup weka kwenye treya ya kupikia tandaza na uma ili upate matundu juu ya biskuti.
  5. Pika (bake) kwenye oven lenye moto wa 375 F. kwa muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.

KIDOKEZO

 

Unaweza kufanya nusu ya vipimo kwani biskuti zinatokea nyingi.

 

 

 

 

Share