Shaykh Fawzaan: Tofauti Kati Ya Manhaj Na ‘Aqiydah

 

Tofauti Kati Ya Manhaj Na ‘Aqiydah

 

Shaykh Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Je, kuna tofauti baina ya ‘Aqiydah Na Manhaj?

 

 

JIBU:

 

Manhaj ina maana pana zaidi kuliko ‘Aqiydah.

Manhaj inapatikana katika ‘Aqiydah na katika maadili na tabia na muamala; na katika maisha yote ya Muislamu. 

Ama ‘Aqiydah hii inatokana na asili (msingi) wa Iymaan pamoja na maana ya Shahada mbili na yanayohusiana nayo. Hii ndio ‘Aqiydah.

 

 

[Al-Ajwibah Al-Mufiydah, uk. 75]

 

Share