Skip navigation.
Home kabah

Qaswida ya 'Mgeni si yule aliyekwenda Shaam na Yemen'




Imetungwa na Zaynul-'Abidiyn 'Aliy Bin Al-Husayn bin 'Aliy bin Abi Twaalib


قصيدة ليس الغريب – زين العابدين علي بن الحسين رحمه الله

Qaswida ya 'Mgeni si yule aliyekwenda Sham na Yemen'

 

 

 

لَيْسَ الغَريبُ غَريبَ الشَّامِ واليَمَنِ                      إِنَّ الغَريبَ غَريبُ اللَّحدِ والكَفَنِ

Mgeni si yule aliyekwenda Sham au Yemen, bali mgeni hasa ni yule wa mwanandani wa kaburi na sanda.

إِنَّ الغَريِبَ لَهُ حَقٌّ لِغُرْبَتـِهِ                              على الْمُقيمينَ في الأَوطــانِ والسَّكَنِ

Bila shaka mgeni kwa ugeni wake, ana haki ya kukirimiwa na wenyeji wake katika nchi na makazi
سَفَري بَعيدٌ وَزادي لَنْ يُبَلِّغَنـي                           وَقُوَّتي ضَعُفَتْ والمـوتُ يَطلُبُنـي

Safari yangu ni ndefu na masurufu yangu hayatonifikisha popote, na nguvu zangu zimedhoofu huku mauti yakiniandama


وَلي بَقايــا ذُنوبٍ لَسْتُ أَعْلَمُها                         الله يَعْلَمُهــا في السِّرِ والعَلَنِ

Nina mabaki ya madhambi na mimi siyajui, Mwenyezi Mungu Anayajua nikiyafanya kwa siri au hadharani


مـَا أَحْلَمَ اللهَ عَني حَيْثُ أَمْهَلَني                         وقَدْ تَمـادَيْتُ في ذَنْبي ويَسْتُرُنِي

Ni upole ulioje Anaonifanyia Mwenyezi Mungu pale Anapoendelea kunipa muda, wakati mimi nimezamia kwenye madhambi Naye Ananisitiri


تَمُرُّ سـاعـاتُ أَيّـَامي بِلا نَدَمٍ                          ولا بُكاءٍ وَلاخَـوْفٍ ولا حـَزَنِ

Masaa ya umri wangu yanapita bila mimi kujuta, wala kulia, wala kuogopa na wala hata kuhuzunika


أَنَـا الَّذِي أُغْلِقُ الأَبْوابَ مُجْتَهِداً                        عَلى المعاصِي وَعَيْنُ اللهِ تَنْظُرُنـي

Mimi ndiye ninayejifungia kwa hima milango ya maasi, na ilhali Jicho la Mwenyezi Mungu linanitizama


يَـا زَلَّةً كُتِبَتْ في غَفْلَةٍ ذَهَبَتْ                           يَـا حَسْرَةً بَقِيَتْ في القَلبِ تُحْرِقُني

Ee dhambi lililoandikwa, limekwenda bila kuhisi, ee majuto yaliyosalia moyoni yakiniunguza


دَعْني أَنُوحُ عَلى نَفْسي وَأَنْدِبُـهـا                     وَأَقْطَعُ الدَّهْرَ بِالتَّذْكِيـرِ وَالحَزَنِ

Niache niililie na niiombolezee nafsi yangu, na niumalize umri wangu wote kwa kukumbusha na kuhuzunika


كَأَنَّني بَينَ تلك الأَهلِ مُنطَرِحــَاً                         عَلى الفِراشِ وَأَيْديهِمْ تُقَلِّبُنــي

Kama kwamba mimi nimejibwaga kitandani katikati ya watu hao, huku mikono yao ikinigeuzageuza


وَقد أَتَوْا بِطَبيبٍ كَـيْ يُعالِجَنـي                         وَلَمْ أَرَ الطِّبَّ هـذا اليـومَ يَنْفَعُني

Na nikaletewa tabibu ili aniponyeshe, wala sikuona tabibu wa kunifaa siku hii

واشَتد نَزْعِي وَصَار المَوتُ يَجْذِبُـها                      مِن كُلِّ عِرْقٍ بِلا رِفقٍ ولا هَوَنِ

Kung’olewa roho kumekuwa kugumu na kuzito, na mauti yamekuwa yakiivuta, toka kwenye kila mshipa bila huruma wala upole


واستَخْرَجَ الرُّوحَ مِني في تَغَرْغُرِها                    وصـَارَ رِيقي مَريراً حِينَ غَرْغَرَني

Mauti yakaitoa roho yangu kwa mkoromo wake kooni, na mate yakawa machungu yaliposakama kooni.


وَغَمَّضُوني وَراحَ الكُلُّ وانْصَرَفوا                       بَعْدَ الإِياسِ وَجَدُّوا في شِرَا الكَفَنِ

Wakanifunga macho kisha wote wakaondoka, baada ya kukata tamaa na wakafanya hima ya kununua sanda


وَقـامَ مَنْ كانَ حِبَّ لنّاسِ في عَجَلٍ                   نَحْوَ المُغَسِّلِ يَأْتينـي يُغَسِّلُنــي

Na yule aliyekuwa akinipenda zaidi akasimama haraka, kwenda

kuniletea mwoshaji wa kuniosha


وَقــالَ يـا قَوْمِ نَبْغِي غاسِلاً حَذِقاً                   حُراً أَرِيباً لَبِيبـاً عَارِفـاً فَطِنِ

Akasema: Enyi watu wangu! Tunataka mwoshaji mmakinifu,

hodari, mwerevu, mjuzi na stadi


فَجــاءَني رَجُلٌ مِنْهُمْ فَجَرَّدَني                       مِنَ الثِّيــابِ وَأَعْرَاني وأَفْرَدَني

Hapo akaja mtu kati yao, akanivua nguo na kuniacha uchi

bila chochote


وَأَوْدَعوني عَلى الأَلْواحِ مُنْطَرِحـاً                    وَصـَارَ فَوْقي خَرِيرُ الماءِ يَنْظِفُني

Kisha wakanipeleka wakanibwaga juu ya vibao, na pakawa juu yangu

sauti ya maji yanayonisafisha


وَأَسْكَبَ الماءَ مِنْ فَوقي وَغَسَّلَني                    غُسْلاً ثَلاثاً وَنَادَى القَوْمَ بِالكَفَنِ

Akanimiminia maji juu yangu, akiniosha mara tatu tatu na

kuwanadia watu walete sanda


وَأَلْبَسُوني ثِيابـاً لا كِمامَ لهـا                     وَصارَ زَادي حَنُوطِي حيـنَ حَنَّطَني

Wakanivalisha nguo isiyo na mikono, na masurufu yangu yakawa ni dawa ya kuzuia nisinuke anayonipaka mwoshaji


وأَخْرَجوني مِنَ الدُّنيـا فَوا أَسَفاً                  عَلى رَحِيـلٍ بِلا زادٍ يُبَلِّغُنـي

Kisha wakaniondosha duniani, ee majuto ya kusafiri bila kuwa na masurufu ya kunifikisha niendako.


وَحَمَّلوني على الأْكتـافِ أَربَعَةٌ                      مِنَ الرِّجـالِ وَخَلْفِي مَنْ يُشَيِّعُني

Wakanibeba watu wanne mabegani, na nyuma yangu wakafuata wanaokwenda kunizika


وَقَدَّموني إِلى المحرابِ وانصَرَفوا                   خَلْفَ الإِمـَامِ فَصَلَّى ثـمّ وَدَّعَني

Wakanifikisha kwenye mihrabu, kisha wakasimama nyuma ya Imamu, akaniswalia kisha akaniaga.


صَلَّوْا عَلَيَّ صَلاةً لا رُكوعَ لهـا                      ولا سُجـودَ لَعَلَّ اللـهَ يَرْحَمُني

Wakaniswalia Swalah isiyo na rukuu wala sijda, ili pengine

Mwenyezi Mungu Akanirehemu


وَأَنْزَلوني إلـى قَبري على مَهَلٍ                    وَقَدَّمُوا واحِداً مِنهـم يُلَحِّدُنـي

Wakaniteremsha taratibu kaburini mwangu, na wakamtanguliza mmoja wao anilaze kwenye mwanandani

وَكَشَّفَ الثّوْبَ عَن وَجْهي لِيَنْظُرَني                  وَأَسْكَبَ الدَّمْعَ مِنْ عَيْنيهِ أَغْرَقَني

Akanifunua uso ili anitizame, na machozi yanayobubujika

machoni mwake yakanilowesha.


فَقامَ مُحتَرِمــاً بِالعَزمِ مُشْتَمِلاً                    وَصَفَّفَ اللَّبِنَ مِنْ فَوْقِي وفـارَقَني

Akasimama kwa heshima na azma kamili, akapanga matofali

juu yangu kisha akaniacha.


وقَالَ هُلُّوا عليه التُّرْبَ واغْتَنِموا                   حُسْنَ الثَّوابِ مِنَ الرَّحمنِ ذِي المِنَنِ

Kisha akasema: Haya mmiminieni mchanga, na ziwahini thawabu njema toka kwa Mwenyezi Mungu Mrehemevu na Mwenye wema.


في ظُلْمَةِ القبرِ لا أُمٌّ هنــاك ولا                  أَبٌ شَفـيقٌ ولا أَخٌ يُؤَنِّسُنــي

Ndani ya giza la kaburi, hakuna huko mama, wala baba wa kunionea huruma wala ndugu wa kuniliwaza


فَرِيدٌ وَحِيدُ القبرِ، يــا أَسَفـاً                     عَلى الفِراقِ بِلا عَمَلٍ يُزَوِّدُنـي

Niko peke yangu kaburini, ee majuto ya kuiacha dunia

bila amali za kunisaidia

 

فَلا تَغُرَّنَّكَ الدُّنْيــا وَزِينَتُها                   وانْظُرْ إلى فِعْلِهــا في الأَهْلِ والوَطَنِ

Basi kamwe dunia na mapambo yake isikudanganye, angalia imewafanya nini watu na nchi.


وانْظُرْ إِلى مَنْ حَوَى الدُّنْيا بِأَجْمَعِها                هَلْ رَاحَ مِنْها بِغَيْرِ الحَنْطِ والكَفَنِ

Hebu mwangalie yule aliyejilimbikizia dunia yote, hakuondoka na chochote isipokuwa dawa ya kuzuia asinuke na sanda yake tu


خُذِ القَنـَاعَةَ مِنْ دُنْيَاك وارْضَ بِها              لَوْ لم يَكُنْ لَكَ إِلا رَاحَةُ البَدَنِ

Kinaika na ridhika na ukipatacho duniani, na kama si hivyo,

basi hutakuwa na raha

 

يا زَارِعَ الخَيْرِ تحصُدْ بَعْدَهُ ثَمَراً                 يَا زَارِعَ الشَّرِّ مَوْقُوفٌ عَلَى الوَهَنِ

Ewe mwenye kupandikiza kheri! Matunda utayachuma baadaye. Ewe mwenye kupandikiza shari! Utasimamishwa juu ya unyonge.

يـَا نَفْسُ كُفِّي عَنِ العِصْيانِ واكْتَسِبِي              فِعْلاً جميلاً لَعَلَّ اللهَ يَرحَمُني

Ewe nafsi! Jizuie na maasia na chuma vitendo vyema, pengine

Mwenyezi Mungu Akanirehemu

 

يَا نَفْسُ وَيْحَكِ تُوبي واعمَلِي حَسَناً             عَسى تُجازَيْنَ بَعْدَ الموتِ بِالحَسَنِ

Ewe nafsi! Kwanini usitubie na ukatenda mema? Huenda

Ukalipwa mema baada ya kufa


ثمَّ الصلاةُ على الْمُختـارِ سَيِّدِنـا               مَا وَصَّـا البَرْقَ في شَّامٍ وفي يَمَنِ

Kisha rehma kwa Bwana wetu mteuliwa, kwa nuru

aliyousia Sham na Yemen


والحمدُ لله مُمْسِينَـا وَمُصْبِحِنَا                  بِالخَيْرِ والعَفْوْ والإِحْســانِ وَالمِنَنِ

Tunamshukuru Mwenyezi Mungu Anayetufikisha jioni na asubuhi, kwa kheri, msamaha, ihsani na wema.