042-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Aliyeingiwa Na Wasiwasi Katika Swalaah Yake Au Kisomo Chake

Hiswnul-Muslim

042-Du’aa Ya Aliyeingiwa Na Wasiwasi Katika Swalaah Yake Au Kisomo Chake

www.alhidaaya.com

 

 

 Bonyeza Hapa Usikilize

 

 

[138]

أَعُوذُ بِاللَّهِ مِنَ الشَّيْطانِ الرَّجِيْمِ

Au’wudhu biLLaahi minash-shaytwaanir-rajiym

 

Najikinga na Allaah kutokana na shaytwaan aliyelaaniwa. (Kisha utatema vijimate vichache upande wa kushoto mara tatu)[1] [yaani kama mwenye kupuliza].

 

 

 

 


[1]Hadiyth ya ‘Uthmaan bin Abi Al-‘Aasw (رضي الله عنه) amesema: Nilimwambia Rasuli (صلى الله عليه وسلم): Ee Rasuli wa Allaah hakika Shaytwaan amenikalia kati yangu na kati ya Swalaah yangu na kisomo changu, ananitatiza.  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) akasema: ((Huyo ni Shaytwaan aitwae Khanzab ukimuhisi amekujia basi muombe Allaah kinga kutokana na [wasiwasi] naye, na tema vijimate vichache kushotoni kwako mara tatu)) Akasema: ”Nikafanya hivyo Allaah akaniondoshea” - Muslim (4/1729) [2203].

 

 

 

Share