Kababu Za Mayai

VIPIMO
Mayai yaliochemshwa 6
Nyama ya kusaga 1 1/2 Ratili (LB)
Tangawizi na thaumu iliyosagwa 1 kijiko cha Supu
Pili pili mbichi ya Kusaga 1
Mafuta 2 Vijiko Vya Supu
Unga wa mahindi (Constarch) 1 Kijiko cha Supu
Chumvi Kisia
Bizari ya manjano 1/4 kijiko cha chai
Dania ya Kusaga 1/4 Kijiko cha chai
Bizari ya Pilau 1/4 Kijiko cha chai
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1.Changanya nyama na vitu vyake kisha gawanya madonge 6 yaliyosawa.
2.Chukuwa donge moja tia ndani yake yai uliochemsha na lifunike vizuri .
3.Ukisha maliza yote panga kwenye treya ya kupikia katika jiko la oveni na zipike kwa moto wa 375F kwa muda wa dakika 25.
4.Yakishaiva epua na kisha ukate
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
