Skip to main content

Wali Wa Samaki Na Mboga

Wali Wa Samaki Na Mboga

VIPIMO VYA SAMAKI

Samaki wa sea bass vipande - 1 1/2  LB (Ratili)

Kitunguu saumu(thomu/galic) -1 Kijiko cha supu

pilipili mbichi iliyosagwa - 1 Kijiko cha chai

Bizari ya manjano au ya pilau - 1/2 Kijiko cha chai

Paprika ya unga au pilipili ya unga - 1 kijiko cha chai

Chumvi - Kiasi

Ndimu

Mafuta - 3 Vijiko vya supu


 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
  1. Roweka samaki kwa viungo hivyo vyote kwa muda wa robo saa hivi.
  1. Washa oven moto wa 400F.
  2. Kisha weka samaki katika trea na choma kwa muda wa dakika 15 na weka moto wa juu dakika za mwisho ili ipate rangi nzuri.
  3. Ikishaiva epua na itakuwa tayari kuliwa.
VIPIMO VYA MBOGA

Gwaru (green beans) - 1 LB

Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 kijiko cha supu

Karoti - 4-5

Chumvi - Kiasi

Bizari ya manjano - 1/2   Kijiko cha chai

Pilipili manga - 1/4 kijiko cha chai

Mafuta ya zaituni - Kiasi


 
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
  1. Kata kata karoti na toa sehemu ya mwisho za binzi.
  2. Weka mafuta katika sufuria kisha kaanga karoti na gwaru
  3. Kisha weka moto mdogo na funika ili ziwive na sio kuvurujika.
  4. Karibu na kuiiva tia thomu kaanga kidogo,tia bizari ,chumvi na pilipili manga.
  5. Ikisha changanyikana vizuri epua na tayari kuliwa na wali na samaki.