Skip to main content

Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika (آداب الزفاف في السنة المطهرة)06-Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika: (Du'aa) Ya Kusema Wakati Wa Kumuingilia Mkeo

Mume anapotaka kumuingilia mkewe, inampasa daima aseme:

بِسْمِ الله اللّهُـمَّ جَنِّبْنا الشَّيْـطانَ، وَجَنِّبِ الشَّـيْطانَ ما رَزَقْـتَنا

Bismillahi, Allaahuuma Jannibnaa-sh-Shaytwaan, Wa Jannibish-Shaytwaana Maa Razaqtanaa

Kwa jina la Allaah, Ee Allaah Tuepushe na Shaytwaan, na Muepushe shaytwaan na Ulichoturuzuku (yaani kizazi).

 

Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amesema kuhusu hili:

((فإن قضى الله بينما ولداً؛ لم يضره الشيطان أبداً))  

((Baada ya hapo Allaah سبحانه وتعالى Akijaalia, watapata mtoto ambaye Shaytwaan hatoweza kumdhuru abadan))[1]

 

[1] Al-Bukhaariy