Wameingiliana Baada ya Alfajiri –Nini Hukmu yake ? Na Je, Swawm Inafaa
SWALI:
A.W.W.NAKUTAKIENI KILA KHERI,
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Waislamu wanapaswa kuzingatia
((أُحِلَّ لَكُمْ لَيْلَةَ الصِّيَامِ الرَّفَثُ إِلَى نِسَآئِكُمْ هُنَّ لِبَاسٌ لَّكُمْ وَأَنتُمْ لِبَاسٌ لَّهُنَّ عَلِمَ اللّهُ أَنَّكُمْ كُنتُمْ تَخْتانُونَ أَنفُسَكُمْ فَتَابَ عَلَيْكُمْ وَعَفَا عَنكُمْ فَالآنَ بَاشِرُوهُنَّ وَابْتَغُواْ مَا كَتَبَ اللّهُ لَكُمْ وَكُلُواْ وَاشْرَبُواْ حَتَّى يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ ثُمَّ أَتِمُّواْ الصِّيَامَ إِلَى الَّليْلِ ...))
((Mmehalalishiwa usiku wa Swawm kuingiliana na wake zenu. Wao ni vazi kwenu, na nyinyi ni vazi kwao. Allaah Anajua kwamba mlikuwa mkizikhini nafsi zenu. Kwa hivyo Amekukubalieni toba yenu na Amekusameheni. Basi sasa changanyikeni nao na takeni Aliyokuandikieni Allaah. Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni Swawm mpaka usiku.)) [Al-Baqarah: 187]
Sasa vipi muda wote huo usiwe wa kumtosha Muislamu kufanya yote anayoyatamani na kusubiri hadi karibu na Alfajiri ndio atake kufanya? Kwa nini usifanye hima ya kujiwekea saa ukahakikisha kuwa utaamka muda wa kutosha
Ikiwa hukujua hakika kuwa wakati wa Alfajiri umewadia unatakiwa ulipe siku hiyo na uombe maghfirah kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala). Lakini ikiwa ulijua au ulikuwa una hisia kuwa wakati umekwisha lakini tendo lile likawa limekukolea hadi ukashindwa kujizuia, basi itabidi ulipe kafara yake. Na mkeo ikiwa alitaka mwenyewe kujimai nawe pia naye itabidi atimize kafara hiyo na ikiwa ulimlazimisha basi yeye atakuwa hana kafara hiyo ila tu ailipe siku hiyo moja.
Haipasi kufanya mchezo na amri za Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) na Mjumbe wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) khaswa katika mwezi huu mtukufu, kwani amri kama hizo ukienda nazo kinyume basi utapata matatizo duniani na akhera, na matatizo ya kidunia ni kama hayo ya kulipa kafara ambayo si rahisi na wengi hawawezi kuitekeleza.
Tunawapa nasaha ndugu zetu Waislamu wote katika mwezi huu wawe na tahadhari kubwa kufanya kinyume na ipasavyo ili kujiepusha na dhambi, kulipa kafara na kubakisha Swawm zenu katika usalama wake.
Ingia katika viungo vifuatavyo usome maelezo zaidi ya hukmu zake:
Alifanya Jimai (Kitendo Cha Ndoa) Bila Ya Kujua Kwamba Alfajiri Imeingia
Kufanya Jimai Katika Mwezi Wa Ramadhaan
Kitendo Cha Ndoa Wakati Wa Ramadhaan
Hizi ni Fataawa zote zinazohusu Kafara ya Swawm:
Na Allaah Anajua zaidi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


