Damu Ya Hedhi Inayotokeza Na Kurudi Afunge Swawm?

 

SWALI: 

Tafazalini naomba muni fafanuliye aya yafuatayo.

 Nikiwa kati ya hli ya kike kuna muda damu inasima kisha tena inarudi kutoka.na hiyi hali ina nisumbuwa sanakama tuko katika huwu mwezi wa ramadhani. Masalani kawaida huwa na fanya siku 4 lakini hapa kati kuna siku 1hedhi in kuwa imesima sasa hiyi siku yenye imesimama nitafanya aje nitafunga ama nitasubiri nijitwaharishe?

Nina shukuru kwa yote.

 


 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa dada yetu kwa swali hilo muhimu kuhusu damu ya ada iliyo na utata kama ulivyoeleza. Ama kuhusu hilo yapo mambo ambayo tunafaa tuyaangalie ili tupate hukumu muafaka. Mambo yenyewe ni kama yafuatayo:

 

1.      Utajaribu kwanza kutofautisha baina ya damu yako ya hedhi na damu nyengineyo, utaangalia hii damu ikiwa rangi, harufu na twabia (maumbile) yake ni kama ya hedhi au ni tofauti. Ikiwa ni kama ya hedhi basi utabaki umekatazwa kuswali, kufunga na kujimai na mumeo kama ulivyokuwa kwani hakuna muda maalumu wa mwisho wa hedhi, ingawa Maulamaa wengine wameweka mpaka wa siku kumi na tano (15). Ukipata damu ni kinyume na kawaida ya hedhi yako, utaoga na kuswali kwani hiyo haitakuwa ni ada ya hedhi yako.

2.      Ikiwa huwezi kutofautisha baina ya hedhi na damu nyengineyo, na jambo hili linapatikana kwa wanawake wengi, utabaki katika hali ya hedhi. Hivyo, hutaswali, hutafunga wala kujamiiana na mumeo mpaka utwahirike kwani hakuna mipaka ya muda kwa damu ya hedhi.

3.      Ama ule umanjano na kufifia kwa rangi ni maji anayoona mwanamke kama usaha na umanjano wake umeiva. Mwanamke anapoona hii baada ya kukatika damu au baada ya kukauka, haichukuliwi kuwa ni hedhi, naye atakuwa twahara. Kwa hiyo, ataswali, atafunga na kuweza kujamiiwa na mumewe. Hiyo ni kwa mujibu wa Hadiyth ya Umm ‘Atwiyah (Radhiya Allaahu ‘anha) aliyesema: “Tulikuwa hatuchukulii fifia kwa rangi na umanjano chochote” (Abu Daawuud, an-Nasaa’iy na Ibn Maajah).

Kwa maelezo zaidi bonyeza viungo vifuatavyo upate maswali na majibu yenye mas-ala kama haya:

Damu Ya Hedhi Inayoendelea Kwa Muda Mrefu

Istihaadhwah (Damu Inayoendelea baada ya Hedhi) Na Hukumu Zake

Na Alaah Anajua zaidi

 

 

 


Share