Tumesikia na Tunatii
‘Abdun-Naaswir Hikmany
Kuna njia moja na njia moja tu inayoweza kutuwezesha kupata mafanikio. Imani ya Uislamu! Ni imani ndio iliyowasaidia Waislamu wa kale na bado inabaki kuwa ni nguvu pekee ambayo itakisaidia kizazi cha leo. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anatuamrisha kufuata njia hiyo:
{{Na kwa hakika hii ndiyo Njia yangu Iliyo Nyooka. Basi ifuateni, wala msifuate njia nyingine, zikakutengeni na Njia Yake. Haya Amekuusieni ili mpate kumcha Mungu}} [Al-Aaraf: 153]
Nafasi na matatizo yetu ya leo sio tofauti na yale yaliyowakuta Waislamu wa kale. Walikuwa ni wachache lakini waliweza kufanikiwa na kuwashinda hata Warumi na Wafursi. Hao Warumi na Wafursi walikuwa na nguvu za kijamii, kisiasa na kiuchumi. Juu ya hivi, muujiza mkubwa ni kwamba waliwashinda Kaizari na Kosroisi sio zaidi ya miaka 50 tu. Yote haya yalifanyikaje? Si chengine ila ni imani
Njia iliyonyooka ya Uislamu haipitiki kwa kuwa Muislamu pekee tu. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anatusisitiza kufanya amali za kumnyenyekea Allaah sio kwetu sisi tu, bali pia kuwahimiza vizazi vyetu kushikamana na njia hii:
“Fanyeni amali katika kumtii Allaah na ogopeni kumuasi Allaah, waamrisheni watoto wenu kufuata amri na kuacha makatazo, kwani
Kwanini hatuna nguvu za kutosha kuuhami Uislamu wetu angalau kwa vitendo vyetu? Ajabu tunasimama na kumuomba Mola wetu mara 17 kwa siku Atuongoze njia iliyonyooka na hali ya kuwa hatujafunua nyoyo zetu kuhitajia huo muongozo. Tunatamka kwamba Yeye Ndiye tunayemuabudia na Yeye tu Ndiye tunayemuomba mara 17 kwa siku. Lakini bado tu, hauonekani uwiano baina ya maombi yetu na wajibu wetu wa kuuhami Uislamu.
Tukumbuke kwamba njia ya Uislamu tuliyoichagua haitotupatia mafanikio kiurahisi kwa kuwa tu ni Waislamu huku tukiwa tunacheza miziki, , kunywa pombe, kuzini, kula riba na kadhalika. La hasha! Hiyo siyo njia aliyoamrishwa Muislamu ndani ya Uislamu. Muislamu anayezungumzwa na Uislamu ni yule mwenye kumnyenyekea Muumba wa Mbingu na Ardhi pamoja na kufuata maamrisho yote aliyokuja nayo Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Halikadhalika, tuelewe ya kuwa Dini ya Uislamu tuliyoichagua kwa ridhaa zetu haijatandikiwa maua wala sio njia inayofanana na kitanda cha king size au zulia jekundu red carpet. Isipokuwa Uislamu ni njia inayohitaji kujitolea kwa kujisalimisha mbele ya amri za Muumba. Hivyo Muislamu kwa kujitolea huko awe tayari kutoka majasho na machozi. Kwa hali na
{{Na umuabudu Mola wako hadi ikufikie hiyo yakini (Nayo ni mauti)}} [Al-Hijr: 99]
Uislamu unahitaji hamasa, mashaka na kuwa tayari kwa lolote. Lililo jipya hapa ni lipi? Mbona vyama na jumuiya nyengine zinakuwa na mafanikio? Bila ya shaka mafanikio
Ni kipi cha kufanya ili kutambua kwamba Uislamu ni bora kwetu? Tukielewa fika kwamba Uislamu ni mfumo bora kabisa unaoweza kupatikana duniani kote, na kwamba taariykh, jiografia na nafasi yetu kimataifa inaonesha kwamba tunaweza kurudia heshima, uongozi na haki kwenye dunia hii. Basi ni imani ndiyo itakayotufanya kutambua nafasi yetu ndani ya dunia hii. Imani ambayo inapatikana kwa kukaa kitako kusoma Qur-aan na Sunnah pamoja na kuzifanyia kazi kanuni zilizomo humo.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


