Anaweza Kumlipia Mumewe Gharama Za Kwenda Hijjah?

SWALI:

assalaam alaykum warahmaturllaah taallah  wabarakatu.namshukuru mwenyeezi mungu mtukufu aliyewapa uwezo wa kutuelimisha.ninamuomba mola wetu mtukufu awajaalie kila la kheri.nashukuru jibu lenu mlilonijibu limezaa matunda mema mwenyeezi mungu mtukufu awatilie wepesi. kwani kutokana na ushauli wenu nikaenda kumlingania mme wangu.alhamdu lillaah rabbi l'alamiina sasa ameacha pombe na anaswali swala tano. mwenyeezi mungu mtukufu awabarikiinshaallah amiin!.

 

sasa swali langu naweza kwenda naye hijja kwa gharama zangu?.

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

 

Tunashukuru kujua kwamba nasaha zetu zimekusaidia na umeweza kuwa sababu ya kuongoka mumeo kwa idhini ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala). Inapasa umshukuru Mola Mtukufu kwani Yeye Ndiye Mwenye kuwahidi waja Wake, sisi ni njia tu za kupitia kupata uongofu kama huo.

 

 

 

Ama kuhusu kumlipia kwenda Hajj, na kwenda naye pamoja, inafaa ikiwa unao uwezo na umependa mwenyewe. Hili ni jambo jema kabisa khaswa kwa vile mumeo alitoka kwenye maasi na kuingia katika twaa'a (Uchaji Allaah). Kwa hiyo ni vizuri kukimbilia kutekeleza ibada/fardhi hiyo muhimu ili Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Azidi kumuongoza katika njia iliyonyooka.

 

 

 

Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Awazidishie iymaan ya dini Yenu na mzidi kubakia katika ridhaa Yake Mola Mtukufu.

 

 

 

Na Allaah Anajua

 

 

Share