Kusafiri Peke Yake Bila Ya Mahram Na Kusomewa Qur-aan Kwa Muda Mrefu Kwa ajili ya Matibabu?
SW
Assalam Aleylum. Sheykh ninaumwa na ninataka kwenda nchi ya Kiislamu kusomewa qur'ani. Na sina mahram ninawesa kusafiri peke yangu??? Na mahali napoishe sijapata sheykh wakunisomea natakiwa nisomewe kwa muda mrefu. Assalam Aleykum. [make duua 4 me inshaallah]
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukran zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kufanya safari kwa ajili ya kusomewa. Awali ya yote tunafaa tuelewe kuwa tiba ya Qur-aan ni mwanzo mtu mwenyewe awe ni mwenye kusoma kwani kufanya hivyo kutampatia yeye kinga.
Mbali na
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokataza mwanamke asisafiri bila mahram ni kwa sababu ya zile shida nyingi ambazo anazipata. Nchi ya ugenini ni nchi ya ugeni na hata zile za Kiislamu huenda mwanamke akapata matatizo mengi na hivyo kushindwa kusaidika.
Je, umetafuta matibabu aina nyengine
Tukiweza kupata majibu ya hayo tulioyauliza ndio tunaweza kukupatia nasiha ya kwenda au kutokwenda. Kuwa kusafiri kwako huko ni sawa au haifai.
Kwa muhtasari ni kuwa safari ya mwanamke bila Mahram haifai hata kwenda Hajj seuze safari nyinginezo.
InshaAllaah tuko pamoja nawe kwa du’aa ingawa umetuandikia namba 4 hapo badala ya maneno na hali unauliza jambo muhimu. Kuandika kwa mtindo wa namba si jambo la kistaarabu na pia kunaangusha shakhsiyah ya mtu anayefanya hivyo.
Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Akukhafifishie maradhi yako na Akufutie madhambi yako kwayo, wewe pamoja na Waislamu wote wenye maradhi na matatizo mbalimbali. Aamiyn.
Na Allaah Anajua zaidi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


