Bajia Za Bilingani, Viazi Na Njegere

Bajia  Za Bilingani, Viazi Na Njegere 

Vipimo

Bilingani - 1

Viazi - 2

Njegere za kijani (green peas) - 1 kikombe

Pilipili mbichi - 1

Bizari ya pilau iliyosagwa (cumin powder) - ½ kijiko

Chumvi - kiasi

Unga wa dengu - 1 kikombe

Maji - kiasi

Mafuta ya kukaangia katika karai

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Katakata bilingani bila ya kumenya weka kando.
  2. Menya viazi, katakata vipande virefu virefu kama vya chipsi (French fries)
  3. Chemsha njegere hadi ziwive epua weka kando.
  4. Katakata pilipili mbichi ndogo ndogo sana
  5. Changanya vitu vyote na bizari na chumvi.
  6. Changanya unga wa dengu na maji kiasi kidogo uwe mwepesi.
  7. Teka kidogo mchanganyiko, chovya katika unga wa dengu kisha kaanga katika mafuta ya moto.
  8. Epua, chuja mafuta, zikiwa tayari kuliwa kwa chatine  ya mtindi na ukwaju na zilioko katika viungo vifuatavyo:

Chatine Ya Mtindi Na Nanaa

Sosi Ya Ukwaju

 

Share