SWALI:
Nasikitika
Nawaamabilii neno. wataka uwasikize wao na si wewe. Nimefwatilia baadhi ya itkadi zao nikapata kuwa wana husiana na ahmadiya anjuman BAADHI YA ITIKADI ZAO.
1. WANAAMINI KUWA NABI ISA A.S. AMESULUBIWA NA KUFA NA KUFUFUKA WALA HAKUPAZAW MBINGUNI. ALIFIA HAPA HAPA.
2. UTUME BADO UNGALIKO NA UNABII NDIO UMEKWISHA. NA MTUME WAO NI ELIJAH MOHAMED.
3. HAWAAMINI MIUJZA YA MNGU S.W ALOWAPA MITUME YAKE 4. HAWAAMINI KUWA NABI ADAM A.S ALIKUWA PEPONI NA ILE PEPO ILOTAJWA KWENYE QUR'AN NI BUSTANI LILIOKO BASRA NA BAGHDAD.
5. HAWAAMINI KUWA MAJINI NI VIUMBE
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa mchango wako kuhusu Qadiyani.
Hakika Muislamu hafai kuwaita hao Maqadiyani kuwa ni Ahmadiya. Wao wanataka waitwe hivyo ili Waislamu wasiweze kuwatambua na hivyo kuwafuata kwani
Hakika hawa ni watu wabaya kabisa kwani wana sifa nyingine mbali na hizo ulizotaja. Mfano ni:
Ni nasaha kwako uendelee na Da‘wah ya kuwaelezea hao ndugu zetu huenda wakaja kuwafahamu na kuwaacha.
Na soma na wafikishie makala hizi zilizomo ndani ya ALHIDAAYA kuhusiana na kundi
Jihadhari Na Kundi La Ahmadiya (Maqadiyani) Dhidi Ya Uislam
Tunakutakiwa kila la kheri katika ulinganizi wako huo na ujira wako uko kwa Allaah Aliyetukuka.
Na Allaah Anajua zaidi