Jihadhari Na Kundi La Ahmadiyah (Qadiyani) Dhidi Ya Uislam

Jihadhari Na Ubaya Wa Kundi La Ahmadiyya Dhidi Ya Uislam

 

 Alhidaaya.com

 

 

Ndugu mpenzi katika Uislam!

 

 

Tunapenda kukutahadharisha na ubaya ulio hatari sana unaokufikia mlangoni kwako wanaojidai kuwa ni waislamu. Watu hawa wenye mipango mizuri wanawapoteza waislamu wa kawaida wasiojua uislamu vyema na kuwaelekeza kwenye Jahanam.

 

 

Mirza Ghulam Ahmad wa Qadiyani alidai kuwa yeye ni nabiy, masihi na Al-Mahdi. Yeye na kundi lake la Ahmadiyya – wamekwishapigwa marufuku kuwa ni makafiri, wasioamini na waislamu wa mataifa yote duniani.

 

 

Ifuatayo ni orodha ya mambo aliyoyaamini Mirza Ghulam Ahmad Qadiyani, mwanzilishi wa kundi hili yamechukuliwa kutoka vitabu vyake mwenyewe:

 

 

 • Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuelewa maana ya Suwrah Al-Zalzalah (Roohani Khazain Juzuu 3 Izala Aliham uk 166-167)

 

 • Quran ni kitabu cha Allaah na maneno yangu (Tangazo lake la tarehe 15 March 1897)

  

 • Rusuli ni watu waongo. (Roohani Khazain Juzuu 3 Izala Aliham uk. 472)

 

 • Ufunuo wa Nabiy Mohammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pia ulikuwa wa makosa (Roohani Khazain Juzuu 3, Izala Auhani uk.378)

 

 • Al-Imam Al-Mahd hatakuja (kabisa) (Roohani Khazain Juzuu 3, Izala Auham uk 378)

 

 • Ufunuo kwa Nabiy Mohammad hakumjulisha chote kuhusu, IBN Maryam, Dajjal, Khair Dajjal, Yajuuj na Majuuj na Dabbatul Ardh (Roohani Khazain Juzuu 3, Izala Auham, uk. 473)

 

 • Khair Dajjal (Ponda wa Dajjal) ni Treni Dabbatul Ardh ni wazuoni wa kiislamu na makasisi wakristu. Roohani Khazain, Juzuu 3, Izala-Auhani uk. 257)

 

 • Nabiy 'Iysa (Masihi) alikuwa akitumia viini macho na alikuwa hodari kwa hilo, (Roohani khazain, Juzuu 3, Izala Auham uk 257)

 

 • Nabiy 'Iysa (Masihi) alikuwa mtoto wa Yusuf Najjar (Yusuf Seremala) (Roohani Khazain, Juzuu 3, Izala Auhani uk. 254)

 

 • ‘Ilikuwaje tabia ya Masihi ('Iysa) – Mlafi, Mlevi, Hakuwa mja wa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) wala hakuwa mcha wa Allaah, wala Mtaabadi, Jeuri, Mbinafsi, Aliyedai Uungu.’ (Maktubat Ahmadiya, Juzuu 3.)

 

 • ‘Familia yake (Nabiy 'Iysa) ilikuwa pia waabudu Allaah na safi, watatu miongoni mwa nyanya zako walikuwa makahaba, na kutokana na damu yao akzaliwa.’ (Roohani Khazain, Juzuu ya 11 uk. 290)

 

 • Brahin-E-Ahmadiya ni kitabu cha Allaah. (Roohani Khazain, Juzuu ya3, Izala Auham uk. 386)

 

 • Miujiza iliyotajwa ndani ya Quran ni viini macho. (Roohani Khazain, Juzuu ya 3, Izala Auhamu uk. 506)

 

 • ’(Hakika tumeishusha hii Quran, karibu na Qadian) kumetajwa ndani ya Qurani takatifu (Roohani Khazain, Juzuu ya 3 Izala Auham uk. 140) Majina ya Makkah, Madina na Qadiyyan yametajwa ndani ya Quran takatifu kwa heshima (Roohani Khazain, Juzuu ya 3 Izala Auhan uk. 140)

 

 • Baitul Fikr (chumba alichokuwa akikaa na kuandika vitabu) ni kama Qaaba takatifu (Na yeyote aingiaye humo yuko katika amani) (Roohani Khazain, Juzuu ya 1, Brahiin Ahmadiya, Juzuu666-667)

 

 • Aya ya Quran isemayo Ni halisi kabisa na maana yake ni msikiti uliojengwa na baba yake Mirza Ghulam. (Tangazo la msaada wa kujenga mnara wa masihi, makusanyo ya matangazo Juzuu 3 uk. 286)

 

 • Mtukufu Nabiy sio wa mwisho na anayefunga milango ya Rusuli (Roohani Khazain, Juzuu ya 3, Izala Auhan uk. 320)

 

 • Kiama na siku ya hukumu si chochote na hakuna kitu kama Kudra (Roohani Khazain,Juzuu ya 3 uk.2 Kichwa cha habari: Toleo la kwanza)

 

 • Jua halitochomoza kutoka magharibi (Roohani Khazain Juzuu ya 3, Izala Auhan, uk. 376)

 

 • Hakuna adhabu ya kaburini. (Roohani Khazain, Juzuu, Izala Auhan uk. 316)

 

 • Tunasukh (kuhama kwa nafsi) Imani ya kihindu ni sahihi. (Roonani Khazain, Juzuu ya 10 uk. 208)

 

 • Quran takatifu imejaa maneno machafu. (Roohani Khazain, Juzuu3, Izala Auhan uk.115-117)

 

 • Ninadai kuwa mimi ndiye masihi anayengojewa ambaye habari zake zimo kwenye utabiri katika vitabu vitakatifu kwamba atatokea siku za mwisho (Roohani Khazain, Juzuu ya 17: “Tuhfa Golravia” uk. 295)

 

 • ‘Mimi ni Adam, mimi ni Huhu, Mimi ni Ibrahim, mimi ni Is-haq, mimi ni Ismail, mimi ni Muwsaa, mimi ni 'Iysa mtoto wa Mariam, mimi ni Mohammad’ (Roohani Khazain, Juzuu ya 22, uk. 521)

 

 • Mimi ni mche wa serikali ya Uingereza niliyejipandikiza mwenyewe na kujilima mwenyewe. (Roohan Khazain, Juzuu ya 13, uk. 350).

 

 • Kutoka nikiwa na umri mdogo hadi sasa nikiwa na umri wa miaka 65 nimekuwa nikishughulika kwa kalamu yangu na ulimi wangu, katika kazi muhimu ya kugeuza mioyo ya waislamu kuelekea mapenzi ya kweli, ukarimu , utu wema kwa ajili ya serikali ya uingereza na kufuta kabisa fikra ya jihad kutoka mioyo ya waislamu wapumbavu. (Roohani khazain, Juzuu 13 uk. 330)

 

 • ‘…………..Kwa ajili ya serikali ya uingereza nimechapisha na kutawanya vikaratasi 50,000,000 katika nchi ya India na nchi nyingine hadi watu wameachilia mbali imani chafu juu ya Jihad.’ (Roohani Khazain, Juzuu ya 15 uk. 119)

 

 •  

  ‘…………..Na ninajua maandishi haya yamewaathiri watu katika nchi hii India na wale waliokula kiapo kwangu, wameunda jumuiya ya Ahmadiya na mioyo yao imejaa ukarimu kwa hii serikali ya Uingeleza …………….Nao wako tayari kwa moyo wote kutoa maisha yao kuitumikia serikali ya Uingereza.

 

 • (Barua ya Mirza kwa serikali ya Uingereza. Tabligh Risalat, Juzuu ya 6 uk. 65)

 

 • ‘Isiyokuwa watoto wa makahaba ambao mioyo yao imefungwa na Allaah, watu wote wanauamini utume wangu.” (Roohani Khazain, Juzuu ya 5-Aina –e-Kamatat-e-Islam, uk. 547)

 

 • Yeyote asiyemwamini Mirza, si mtii kwa Allaah na Nabiy wake na atakwenda motoni. (Tangazo la Mirza, tarehe 25 may 1900)

 

 

Ee ndugu Muislamu!

 

 

Huu ndio sura halisi ya Mirza Ghulam Qadiyani, mwanzilishi wa jumuia ya Ahmadiyya, yeye na wafuasi wake ni watumishi watiifu wa waingereza na mayahudi.Leo bado wanawatimikia mabwana wao. Kwa vile sote tu makafiri na wanaharamu katika macho ya makadiani, wanahifadhi maslahi ya watu wa ulaya kwa kutufanyia ujasusi.

 

 

Makao yao makuu yako London, na kutoka hapo, huwatumia mawakala wao kwa sura ya wahubiri (wa kiislsmu), kwenda nchi mbalimbali duniani. Wamewakusudia waislamu wa kawaida katika Afrika, Ulaya, na Marekani na kwa waislamu wa katikati mwa nchi za Asia. Hujifanya kuwa mabingwa wa uislamu, na hugawa vitabu vyao bure, hutoa fedha na vichocheo vinginevyo ili kuwanasa waislamu wasio hatia.

 

 

Ya Allaah tulinde sote na udanganyifu wa Uqadiyani/Ahmadiyah dhidi ya Uislamu.

 

Share