Vitabu Hivi Vinafaa?

 

 

SWALI:

 

 

Asalam alayku arhamatulahi wabarakatu ndugu zangu wa alhidaaya. Nawaombea mungu awapeni kila la kheri na baraka afya na uhayi mrefu na awalipe kwa pepo ya fardhowsa amin. Swali langu ni kuwa nina vitabu ambavyo nataka kujua kama ni sahihi au sio, majina ya vitabu ni, MKWELI MWAMINIFU JUZU 1 MPAKA YA 4 kilicho tungwa na Kheikh Said Moosa Mohamed Al-Kindy, na kitabu kiitwacho DUA, NYIRADI NA MALIPO YAKE AKHERA NA DUNIANI. Kilicho tungwa na Ustadh Said kh Mkama. Na kitabu kiitwacho KITABU CHA MADUA, kilicho tungwa na Said bin Abdullah Seif l-hatimiy.

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu vitabu ulivyovitaja.

Hakika ukitaka kitabu cha du’aa na adhkaar ambacho kinaaminika na kiko karibu zaidi na usahihi, basi ni kitabu cha Hiswn Al-Muslim ambacho kinapatikana kwa lugha mbalimbali. Unaweza kukipata hapa alhidaaya kwenye kiungo hiki:

 

Hiswnul Muslim

 

Na Allaah Anajua zaidi

Share