Sunni Anaweza Kuolewa Na Shia?

SWALI:

 

Asalam aleykum! Labda nitakua nimekosea mniweeradhi. Mimi nina maswali; je Sunni anaweza kuolewa na Shia?

 
JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu uwezekano wa Msuni kuolewa na Mshia. Awali ya yote hakuna haja kabisa ya kuomba msamaha kwa swali unalouliza kwani hiyo ni haki yako.

 

Pili, hakuna uwezekano wa Msuni kuolewa na Mshia kwa sababu itikadi za hawa wawili zimetofautiana katika misingi ya Dini kwa kiasi kikubwa. Mshia ni mtu ambaye anawatusi Maswahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum) na kuwachafua wake za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kwenda hata kinyume na Qur-aan inayowasifu kwa sifa nzuri kabisa, pamoja na itikadi zao za kishirikina na kufru zilizojaa kwenye vitabu vyao vya kuaminika kama Al-Kaafiy na vinginevyo.

 

Ukweli Juu Ya Al-Kaafiy (Kitabu Cha Hadiyth Cha Kutegemewa Cha Mashia)

 

Kadhaalika, Maimaam wakubwa za kale na wa sasa wamepinga jambo hilo kwa nguvu na kwa hoja mbalimbali, na hata kufikia kusema Suni mwanamme vilevile haipendezi kumuoa mwanamke wa kishia.

 

Soma maelezo ya Maimaam wakubwa kuhusiana na Mashia:

 

Maoni Ya Maimaam Kuhusu Mashia

 

Vilevile bonyeza kiungo kifuatavyo upate maelezo zaidi kuhusu upotofu wa ‘Aqiydah za Mashia:

 

Itikadi Potofu

 

Itikadi Potofu Za “Shia” Kama Ilivyoandikwa Kwenye Vitabu Vyao - 1

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share