Itikadi Potofu Za Shia Kama Zilivyoandikwa Kwenye Vitabu Vyao

Itikadi Potofu Ya Shia Kama Zilivyoandikwa Kwenye Vitabu Vyao

 

www.alhidaaya.com

 

 

1. Hatutamkubali Allaah huyu wala Mtume wake huyo ambaye Khalifa wake ni Abu Bakr [Anwaarun-Nu’maniyyah, Mjadala 2, uk. 278 - Kilichochapishwa Iran].

 

 

2. Mitume wote (‘Alayhimus Salaam) hawapewi utume mpaka wakubali kuamini kwa makosa vitendo vya Allah [Uswuul al-Kaafi, Mjadala 1, uk. 265 - Kilichochapishwa Iran].

 

 

3. Wamesema hawachukuwi jukumu ya kwamba kuamini Qadar na kubarikiwa kunatokamana na Allaah [Uswuul al-Kaafi, Mjalada 1, uk. 293 - Kilichochapishwa Iran].

 

 

4. Ma-Imamu kumi na nne ambao wamelindwa na makosa [Ma’asumiyn] hao hawana cha kuwafananisha nacho katika kufanya makosa yaliotanguliya ama hawakukosa kabisa, wao ni kama Allaah. [Chouda Sitaray, uk. 2 - Kilochapishwa Pakistan].

 

 

5. Hakuna tofauti baina Allaah na ‘Aliy Katika sifa mfano, za Ubwana wa Pete ya Sulaymaan, Ubwana wa siku ya Qiyaamah, Ubwana katika Swiraat [Kivuko cha juu ya moto wa jahannam], Ubwana katika Uwanja, Ubwana wa kuumba majani katika miti, Ubwana wa utundaji matunda, Ubwana wa uteremshaji mvua, Ubwana wa usukumaji wa maji katika mito. [Jila-ul-‘Uyuun, Mjalada 2, uk. 85 - Kilochapishwa Pakistan].

 

 

6. Kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na wajukuu wake wako kila mahala na wanajua kila kitu, Na hili ni umbile lao lililo madhubuti na halitokamani na Allaah. [Jila-ul-‘Uyuun, Mjalada 2, uk. 85 - Kilochapishwa Pakistan].

 

 

7. Allaah Anapozungumzia baraka Anazungumza kwa lugha ya kifursi na Anapozungumziya adhabu huzungumza kwa lugha ya kiarabu. [Taariykh-al-Islaam, uk. 163 - Kilochapishwa Lahore].

 

 

8. Itikadi ya shia wanapotamka shahada ni “La Illaaha ila Allaah, Muhammadur-Rasuulu-Allaah, ‘Aliy Waliyu-Allaah, Wasiyur-Rasuulil-Allaah, Wa Khaliyfatuh bila Fasl.”  [Tuhfa Namaaz Ja’afariyyah, uk. 10 - Kilochapishwa Pakistan].

 

 

9. Mahala popote ndani ya Qur-aan panapotajwa neno “Rabb”, Maana yake ni “’Aliy” [Jila-ul-‘Uyuun, Mjalada 2, uk. 66 - Kilichochapishwa Pakistan].

 

 

10. Qur-aan haitoonekana (haitopatikana) kwa usahihi wake mpaka atakapokuja Imamu Mahdi (Imamu wa 12 wa Shia). [Anwaarun-Nu’maaniyyah, Mjalada 2, uk. 360 - Kilichochapishwa Iran].

 

 

www.alhidaaya.com

Share