Amekula Vidonge Kutoa Mimba Nini Hukmu Yake?

 

SWALI:

 

ASSALAMA ALAEKUM WA RAHMATU LLAHI WA BARAKATU SUALA LANGU LINAHUSU JUU MWANAMKE ALIE KULA VIDONGE KWA AJILI YA KUTOA MIMBA NINI HUKUMU YAKE IFAHAMIKE KUA MWANAMKE ANA AKILI TIMAMU ILLA PENGINE ALIAFANYA HAYA KUVUNJA ALAKATI NA BABA WATOTO WAKE ALIEMUACHA AHSANTENI SANA WA JAZAKUMU LLAH KHEIR.

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mwanamke kutoa mimba.

Haifai kwa mwanamke katika Uislamu kutoa mimba kwani kufanya hivyo ni kuua kiumbe cha Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala), ambacho kimekatazwa kishari’ah kuuliwa ila kwa sababu inayokubalika Kiislamu. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema: “Wala msiue nafsi ambayo Allaah Amekataza isipokuwa kwa haki. Na aliyeuliwa kwa kudhulumiwa basi Tumempa madaraka mrithi wake. Lakini asipite mpaka katika kuua. Kwani yeye anasaidiwa” (al-Israa’ 17: 32).

Na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Kuondoshwa (kuhalikishwa) kwa dunia mbele ya Allaah ni sahali zaidi kuliko kuuliwa kwa Muislamu” (at-Tirmidhiy, an-Nasaa'iy na Ibn Maajah).

 

Uchukivu wa mke kwa aliyekuwa mume wake usimfanye kufanya dhambi kubwa kama la kutoa mimba. Na huko akidhani anamkomoa mume wake wa zamani au kuvunja mahusiano yoyote baina yao, hajui kuwa amejikomoa mwenyewe kwa kuidhulumu nafsi yake na kujiweka pabaya mbele ya Allaah Mtukufu.

Na kwa kuwa tayari ashatoa mimba bila dharura yoyote inayokubaliwa na Shari’ah, anachotakiwa hivi sasa ni arudi kwa Allaah kwa kuomba msamaha wa kikweli kweli. Awe atatimiza masharti haya yafuatayo:

 

1.     Kujiondoa katika maasiya hayo.

2.     Ajute sana katika kufanya kosa hilo.

3.     Aazimie kutolirudia tena kosa hilo.

 

 

Bonyeza kiungo kifautacho upate maelezo zaidi:

 

Kutoa Mimba - Hukmu Na Kafara Yake

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share