Hukmu Ya Kufuga Ndevu

 

 

Hukmu Ya Kufuga Ndevu

 

Kutoka Katika: Swahiyhu Fiqhis Sunnah

 

 

Alhidaaya.com

 

 

Kuachilia ndevu ni wajibu kwa wanaume kwa dalili zifuatazo:

 

 

1- Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameamuru kuziachilia. Amri hii ni ya lazima, kwani hakuna kiashirio chochote kinachoigeuza na kuipeleka katika usunnah. Na kati ya amri hizo ni neno lake Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

 خالفوا المشركين: وفروا اللحى، وأحفوا الشوارب

"Kuweni kinyume na washirikina; fugeni ndevu kwa wingi na punguzeni masharubu"[Hadiyth Sahihi: Imetolewa na Al-Bukhaariy (5892) na Muslim (259)]

 

 

Na neno lake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

 جزوا الشوارب، وأرخوا اللحى، خالفوا المجوس

"Kateni masharubu na ziachilieni ndevu; nendeni kinyume na wanaoabudu moto" [Hadiyth Sahihi: Imetolewa na Muslim (260)]

 

 

2- Ni kwamba kuzinyoa ni sawa na kujifananisha na makafiri kama inavyoonekana katika Hadiyth mbili zilizotangulia.

 

 

3- Ni kwamba kuzinyoa ni sawa na kuubadilisha Uumbaji wa Allaah na kumtii Shaytwaan asemaye:

 

وَلَآمُرَنَّهُمْ فَلَيُغَيِّرُنَّ خَلْقَ اللَّـهِ ۚ  

…na nitawaamrisha watabadili maumbile ya Allaah.”  [An-Nisaa: 119]

 

4- Ni kwamba kuzinyoa ni sawa na kujifananisha na wanawake. Na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amewalaani wanaume wanaojifananisha na wanawake [Hadiyth Sahihi: Imetolewa na Al-Bukhaariy (5885) na At-Tirmidhiy (2935)]

 

 

Na kwa ajili hiyo, Shaykh wa Uislamu amesema:

Na inaharamishwa kunyoa ndevu zake [Kitabu cha “Al-Ikhtiyaaraat Al-Fiqhiyyah” cha ‘Alaau Ddiyn Al-Ba’aly (uk.10). Angalia pia kitabu cha “Al-Furu’u” cha Ibn Muflih (1/291).]

 

Ibn Hazm na wengineo, wamenukulu Ijmaa’ ya 'ulamaa juu ya uharamu wa kunyoa ndevu.

 

 

Je, Inajuzu Kupunguza Ndevu Zilizozidi Mshiko Wa Kiganja?

 

Baadhi ya 'ulamaa wamefuata mwelekeo wa kujuzu kuondosha ndevu zilizozidi mkamato wa kiganja. Wao wameshikilia Hadiyth ya Ibn ‘Umar ambaye wakati wa kuhiji au kufanya ‘Umrah, alikuwa akizikamata ndevu zake, kilichozidi alikuwa akikiondosha.

 

Wamesema: “Yeye ndiye mpokezi wa Hadiyth yenye kuamuru kuachilia ndevu kwa wingi, hivyo basi yeye ndiye ajuaye zaidi upokezi wake!

 

Katika kaulipokezi hii, wao hawana hoja yoyote kwa dalili zifuatazo:

 

1- Kwamba Ibn ‘Umar Allah Amridhie, alikuwa akifanya hivyo wakati anapojifungua na ihraam ya Hija au ‘Umrah, wakati wao (Maulamaa hao) wanalijuzisha hilo nyakati zote.

 

 

2- Kwamba kitendo hiki cha Ibn ‘Umar kimefahamika kutokana na yeye kuliawilisha neno Lake Subhaanah:

مُحَلِّقِينَ رُءُوسَكُمْ وَمُقَصِّرِينَ

 

… wenye kunyoa vichwa vyenu na wenye kupunguza, [Al-Fat-h: 27]

 

Katika ‘amali za Hijjah, kichwa hunyolewa na ndevu hupunguzwa.

 

3- Ni kwamba Swahaba akisema au kutenda kinyume na alivyohadithia, basi kinachozingatiwa ni maneno yake na wala si ufahamu wake wala kitendo chake. Kwani mazingatio ni kile kilichorufaishwa moja kwa moja kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

Na kutokana na yaliyotangulia, lililo sawa ni wajibu wa kuachia ndevu na kutozikata kwa kuutumia ujumuishi wa amri zilizokuja katika Hadiyth sahihi kama vile: "Fugeni kwa wingi…, ziachilieni…, zifanyeni nyingi…." kama walivyoeleka kwa hilo jamhuri ya 'ulamaa. Na Allaah

 

 

Ndiye Ajuaye zaidi.

 

 

 

Share