Kuomba Nguvu Kutokana Na Mizimu

SWALI: 

A.a mashekhe alhamdullilah kwa kupata hii website ya kiislamu kwa kiswahili ALLAH awazidishie imani. SWALI langu ni kuwa je yafaa kuomba mizimu kwa sababu kuna hata mashekhe fulani huenda kwa mizimu kuomba nguvu kutoka kwa mababu zao.


 

JIBU: 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. 

Shukrani kwa swali lako kuhusu mashekhe kwenda mizimuni na kuomba nguvu kutoka kwa mababu.

Hakika ni maarufu kuwa mwenye kuombwa ni Allaah Aliyetukuka pekee. Ikiwa mtu atamuomba mwengine yeyote hiyo itakuwa ni shirki tena kubwa yenye kumtoa mtu katika Uislamu.

Allaah Aliyetukuka Anasema:

Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada” (al-Faatihah [1]: 5). Hivyo, wa kuombwa na Allaah Aliyetukuka peke Yake. 

Kwa hiyo, suala la kuomba mizimu haifai katika shari’ah yetu ya Kiislamu hata ikiwa inafanywa na anayejiita au kujidai ni shekhe.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share