Neema Za Jannah (Pepo) Tuliyoahidiwa

Neema Za Jannah (Pepo) Tuliyoahidiwa

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Maelezo ya Neema za Jannah (Pepo) tuliyoahidiwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) yametajwa mno katika Qur-aan na Hadiyth.  Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 

إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ مَفَازًا ﴿٣١﴾حَدَائِقَ وَأَعْنَابًا ﴿٣٢﴾وَكَوَاعِبَ أَتْرَابًا ﴿٣٣﴾وَكَأْسًا دِهَاقًا ﴿٣٤﴾لَّا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا وَلَا كِذَّابًا ﴿٣٥﴾جَزَاءً مِّن رَّبِّكَ عَطَاءً حِسَابًا ﴿٣٦﴾

 

“Hakika wenye taqwa watapata mafanikio. Mabustani na mizabibu. Na wanawake wenye vifua vya kujaa wa hirimu moja.Na kikombe kilojaa pomo mvinyo. Hawatosikia humo upuuzi na wala kukadhibisha. Jazaa kutoka kwa Rabb wako, tunukio la kutosheleza” [An-Nabaa: 31-36]

 

Anasema tena (Subhaanahu wa Ta'aalaa) katika Suwratul-Waaqiah:

 

 

وَالسَّابِقُونَ السَّابِقُونَ ﴿١٠﴾أُولَـٰئِكَ الْمُقَرَّبُونَ ﴿١١﴾فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ ﴿١٢﴾ثُلَّةٌ مِّنَ الْأَوَّلِينَ ﴿١٣﴾وَقَلِيلٌ مِّنَ الْآخِرِينَ ﴿١٤﴾عَلَىٰ سُرُرٍ مَّوْضُونَةٍ ﴿١٥﴾مُّتَّكِئِينَ عَلَيْهَا مُتَقَابِلِينَ ﴿١٦﴾يَطُوفُ عَلَيْهِمْ وِلْدَانٌ مُّخَلَّدُونَ ﴿١٧﴾بِأَكْوَابٍ وَأَبَارِيقَ وَكَأْسٍ مِّن مَّعِينٍ ﴿١٨﴾لَّا يُصَدَّعُونَ عَنْهَا وَلَا يُنزِفُونَ ﴿١٩﴾وَفَاكِهَةٍ مِّمَّا يَتَخَيَّرُونَ ﴿٢٠﴾وَلَحْمِ طَيْرٍ مِّمَّا يَشْتَهُونَ ﴿٢١﴾وَحُورٌ عِينٌ ﴿٢٢﴾كَأَمْثَالِ اللُّؤْلُؤِ الْمَكْنُونِ ﴿٢٣﴾جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٢٤﴾

 

“Na waliotangulia mbele, watatangulia mbele. Hao ndio watakaokurubishwa. Katika Jannaat za taanisi. Kundi kubwa katika wa awali. Na wachache katika wa mwishoni. (Watakuwa) Juu ya makochi ya fakhari yaliyotariziwa na kutonewa vito vya thamani kwa ustadi wa hali ya juu. Wakiegemea juu yake wakikabiliana. Watazungukiwa na vijana wenye kudumu. Kwa bilauri na mabirika na vikombe vya mvinyo kutoka chemchemu inayobubujika. Hawatoumizwa vichwa kwavyo na wala hawatoleweshwa. Na matunda watakayopendelea. Na nyama za ndege katika watakazozitamani. Na mahuwr, wanawake wazuri wa Jannah wenye macho ya kupendeza. Kama mfano wa lulu zilizohifadhiwa. Jazaa kwa yale waliyokuwa wakitenda.” [Al-Waaqi’ah: 10-24]

 

 

Suwrah hiyo tukufu inaendelea kutaja Neema za Jannah:

 

لَا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا وَلَا تَأْثِيمًا ﴿٢٥﴾إِلَّا قِيلًا سَلَامًا سَلَامًا ﴿٢٦﴾وَأَصْحَابُ الْيَمِينِ مَا أَصْحَابُ الْيَمِينِ ﴿٢٧﴾فِي سِدْرٍ مَّخْضُودٍ ﴿٢٨﴾وَطَلْحٍ مَّنضُودٍ ﴿٢٩﴾وَظِلٍّ مَّمْدُودٍ ﴿٣٠﴾وَمَاءٍ مَّسْكُوبٍ ﴿٣١﴾ وَفَاكِهَةٍ كَثِيرَةٍ ﴿٣٢﴾لَّا مَقْطُوعَةٍ وَلَا مَمْنُوعَةٍ ﴿٣٣﴾وَفُرُشٍ مَّرْفُوعَةٍ ﴿٣٤﴾إِنَّا أَنشَأْنَاهُنَّ إِنشَاءً ﴿٣٥﴾فَجَعَلْنَاهُنَّ أَبْكَارًا ﴿٣٦﴾عُرُبًا أَتْرَابًا ﴿٣٧﴾لِّأَصْحَابِ الْيَمِينِ ﴿٣٨﴾ثُلَّةٌ مِّنَ الْأَوَّلِينَ ﴿٣٩﴾وَثُلَّةٌ مِّنَ الْآخِرِينَ ﴿٤٠﴾

 

 

“Hawatosikia humo upuuzi na wala yanayosababisha dhambi. Isipokuwa itasemwa: Salama, salama!  Na watu wa kuliani, je, ni nani watu wa kuliani? (Watakuwa) miongoni mwa mikunazi iliyokatwa miba. Na migomba ya ndizi iliyopangwa matabaka. Na kivuli kilichotandazwa. Na maji yenye kumiminwa. Na matunda mengi. Hayana kikomo na wala hayakatazwi. Na matandiko ya kupumzikia yaliyoinuliwa. Hakika Sisi Tunawaanzisha (huwrun-’iyn) uanzishaji. Tunawafanya mabikra. Wenye mahaba, ashiki na bashasha kwa waume zao, hirimu moja. Kwa ajili ya watu wa kuliani. Kundi kubwa katika wa awali. Na kundi kubwa katika wa mwishoni.[Al-Waaqi’ah: 25-40]

 

Wa kwanza kuingia Jannah ni Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kama alivyosema:

 

 ((آتي الجنةَ فأستفتحُ - أي فأستأذن - فيقولُ الخازنُ : من أنتَ ؟ فأقول : أنا محمد !! فيقول : بِكَ أُمرت ألا أفتحَ لأحدٍ قبلكَ (( أخرجه الإمام مسلم في صحيحه 

 

((Nitafika (katika mlango wa)  wa Jannah nitaomba idhini ya kuingia, atasema milinzi: Nani wewe? Nitasema: Mimi ni Muhammad. Atasema: Kwako nimeamrishwa wala sikuamrishwa nimfungulie mtu mwingine kabla yako)) [Muslim]

Tutazame baadhi ya Hadiyth chache miongoni mwa nyingi zinazosimulia neema za Jannah:

 

 

Daraja yake:
 

عن أبي سعيد الخدري عن النبي صلى الله عليه و سلم قال: ((إن في الجنة مئة درجة، ولو أن العالمين اجتمعوا في إحداهن وسعتهم)) رواه أحمد بن حنبل في مسنده

 

Kutoka kwa Abu Sa'iyd al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika katika Jannah kuna daraja mia. Na lau kama walimwengu wangelikusanyika katika mojawapo wangeenea) [Ahmad bin Hanbal katika Musnad yake]

 

 

عن أبي هريرة عن النبي صلى الله عليه و سلم قال: ((إن في الجنة مئة درجة أعدها الله للمجاهدين في سبيله، بين كل درجتين كما بين السماء و الأرض، فإذا سألتم الله فاسألوه  الفردوس...إلخ)) رواه البخاري

 

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Katika Jannah kuna daraja mia ambazo Ameziahidi Allaah kwa wanaopigana Jihaad kwa ajili Yake, baina ya kila daraja mbili kama (masafa ya) baina mbingu na ardhi, kwa hivyo, mnapomuomba Allaah Mumuombe (pepo ya) Al-Firdaws)) [Al-Bukhaariy]

 

 

Hakuna uchafu humo:

 

  قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( إن أول زمرة يدخلون الجنة على صورة القمر ليلة البدر ، ثم الذين يلونهم على أشد كوكب دري في السماء إضاءة ، لا يبولون ولا يتغوطون ، ولا يتفلون ولا يمتخطون ، أمشاطهم الذهب ، ورشحهم المسك ، ومجامرهم الألوة -a الألنجوج ، عود الطيب - وأزواجهم الحور العين ، على خلق رجل واحد ، على صورة أبيهم آدم ، ستون ذراعا في السماء(( البخاري

 

Amesema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Kundi la mwanzo watakaongia Jannah watakuwa kama mwezi unapokuwa kamili. Kisha watafuatia ambao watakuwa kama nyota zinazong’ara mbinguni. Hawatakojoa, wala hawatofanya haja kubwa, wala  hawatotema mate, wala hawatopenga kamasi,  vitana vyao vya dhahabu na jasho lao litanukia kama  misk,  vyetezo vyao watatumia udi wa mawardi, wake zao watakuwa ni  Huwrul-‘Ayn wenye macho makubwa. Watu watakuwa katika umbo la aina ya mtu mmoja, la baba yao Aadam (wakiwa) nchi sitini kwa urefu)) [Al-Bukhaariy]   

 

 

Mito yake:

 

 

عَنْ حَكِيم بْن مُعَاوِيَة عَنْ أَبِيهِ قَالَ سَمِعْت رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُول: (( فِي الْجَنَّة بَحْر اللَّبَن وَبَحْر الْمَاء وَبَحْر الْعَسَل وَبَحْر الْخَمْر ثُمَّ تَشَقَّقُ الْأَنْهَار مِنْهَا بَعْد)) وَرَوَاهُ التِّرْمِذِيّ

 

Imetoka kwa Hakiym bin Mu'aawiyah kutoka kwa baba yake ambaye amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Katika Jannah, kuna bahari ya maziwa, na bahari ya maji, na bahari ya asali na bahari ya ulevi (wenye ladha)) kisha mito itafunguka humo)) [At-Tirmidhiy]

 

 

Baada ya kutambua sifa chache hizo za Jannah yenye Neema, tunatumai kwamba tutajitahdi kufanya mema mengi ili tujaaliwe kuingia Jannah (Peponi) ambako maisha yake ni ya kudumu milele kwa furaha na amani.

 

 

Share