Skip navigation.
Home kabah

Ukimkumbuka Allaah Naye Atakukumbuka (Fadhila Za Dhikru-Allaah)


1 Dhul-Hijjah 1427 - 22-12-2006

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):

((فَاذْكُرُونِي أَذْكُرْكُمْ وَاشْكُرُواْ لِي وَلاَ تَكْفُرُونِ))

((Basi nikumbukeni Nitakukumbukeni, na nishukuruni wala msinikufuru)) [Al-Baqarah: 153]

 

Je, kuna mbora zaidi ya Mola wetu Mtukufu tunayemhitaji atukumbuke? Bila shaka hakuna, kwani Yeye Ndiye tunayemhitaji kwa mambo yetu yote ya maisha, duniani na Akhera. Hivyo basi tujitahidi kumkumbuka hasa katika siku hizi tukufu ambazo kama tulivyobainisha katika Nasiha ya Ijumaa iliyopita kuwa ni 'Siku Kumi Bora Kabisa Za Allah'.

Naye (Subhaanahu wa Ta'ala)  Ametuamrisha tumkumbuke sana kila wakati kwani Yeye Ndiye Anayeturuzuku neema na fadhila zote. Naye Anatupa moyo na matumaini kuwa, tutakapomkumbuka Naye Atatukumbuka, Atazidi kutuongoza, Atatuswalia (Atatupa rehema Zake) Yeye na Malaika Wake, na Atatulipa malipo mema mengi duniani na Akhera. Anasema (Subhaanahu wa Ta'ala):

  يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا اللَّهَ ذِكْرًا كَثِيرًا ﴿41﴾ وَسَبِّحُوهُ بُكْرَةً وَأَصِيلًا ﴿42﴾ هُوَ الَّذِي يُصَلِّي عَلَيْكُمْ وَمَلَائِكَتُهُ لِيُخْرِجَكُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ وَكَانَ بِالْمُؤْمِنِينَ رَحِيمًا ﴿43﴾ تَحِيَّتُهُمْ يَوْمَ يَلْقَوْنَهُ سَلَامٌ وَأَعَدَّ لَهُمْ أَجْرًا كَرِيمًا ﴿44﴾

((Enyi mlioamini! Mdhukuruni Allah kwa wingi wa kumdhukuru))  

((Na mtakaseni asubuhi na jioni))

((Yeye na Malaika Wake ndio Wanakurehemuni ili kukutoeni gizani mwende kwenye nuru. Naye ni Mwenye kuwarehemu Waumini))

((Maamkiano yao siku ya kukutana naye yatakuwa: Salama! Na Amewaandalia malipo ya ukarimu)) [Al-Ahzaab: 42-44]

 

'Aliy bin Abi Twalha ameripoti kuwa Ibn 'Abbaas (Radhiya Allahu 'anhu) amesema kuhusu Aayah:

((اذْكُرُوا اللَّهَ ذِكْرًا كَثِيرًا))

((Mdhukuruni Allah kwa wingi wa kumdhukuru))

"Allah Hakuwaamrisha waja Wake kutekeleza wajibu wowote bila ya kuweko mipaka iliyojulikana na Hupokea nyudhuru za wale wasioweza kutekeleza  (wajibu huo). Ama kumdhukuru Allah, Hakuweka mipaka na hakuna atakayekuwa na udhuru wa kutokuweza kumdhukuru Allah isipokuwa atakayedhalilika kwa kupuuza na kudharau, kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema:

 ((فَاذْكُرُواْ اللّهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَى جُنُوبِكُمْ))

((basi mkumbukeni Allah mkisimama, na mkikaa, na mnapojinyoosha kwa kulala)) [An-Nisaa:103]

Kwa maana; usiku na mchana, katika ardhi kavu au baharini, safarini au kubakia nyumbani, katika hali ya utajiri au umasikini, katika hali ya maradhi au katika siha, kwa siri au hadharani – katika hali zote na mazingira yoyote, Allah Anasema:

   ((وَسَبِّحُوهُ بُكْرَةً وَأَصِيلًا))

  ((Na mtakaseni asubuhi na jioni))

Mkifanya hivyo Yeye na Malaika Wake *Watatuswalia" [At-Twabary 20:280]

 

Swalah ya Allah kwa waja Wake ina maana: Anawasifu waja Wake kwa Malaika na pia maana nyingine ni Rahma.

Swalah kutoka kwa Malaika ina maana: ni du'aa zao na kutuombea maghfirah.

Na Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

  ((يقول الله تعالى : أنا عند ظن عبدي بي ، وأنا معه إذا ذكرني ، فإن ذكرني في نفسه ذكرتهُ في نفسي ، وإن ذكرني في ملأ ذكرته في ملأ خير منهم ،وإن تقرب إلى شبراً تقربت إليه ذراعاً ،وإن تقرب إلي ذراعاً تقربت إليه باعاً ، وإن أتاني يمشي أتيتهُ هرولة)) البخاري و سلم

 ((Allah Anasema: Mimi niko mbele ya dhana ya mja Wangu Kwangu, akinitaja moyoni Nami Ninamtaja moyoni na akinitaja katika  kundi, Nami Namtaja  katika kundi bora zaidi ya hilo lake, na akijikurubisha Kwangu paa moja, basi Mimi Najikurubisha kwake kiasi cha dhiraa, na akijikurubisha  Kwangu kiasi cha dhiraa, basi Mimi Nitajikurubisha  kwake kiasi cha kunyoosha mkono hadi kati ya kifua, na akinijia kwa mwendo mdogo basi Nami Nitamjia kwa mwendo wa kasi)) [Al-Bukhaariy na Muslim] 

 

Maonyo Ya Kughafilika kumdhukuru Allah

Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Amewaonya wale ambao nyoyo zao zimeghafilika na kumkumbuka:

 ((فَوَيْلٌ لِّلْقَاسِيَةِ قُلُوبُهُم مِّن ذِكْرِ اللَّهِ أُوْلَئِكَ فِي ضَلَالٍ مُبِينٍ))

((Basi ole wao wenye nyoyo ngumu zisiomkumbuka Allah! Hao wamo katika upotofu wa dhaahiri )) [Az-Zumar:22]

Na Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) naye pia ametuonya katika Hadiyth nyingi, tutataja baadhi yake:

  ((من قعد مقعداً لك يذكر الله فيه كانت عليه من الله ترة ومن اضطجع مضجعاً لم يذكر الله فيه كانت عليه من الله ترة)) ابو داود

((Anayekaa kikao chochote kile asimtaje Allah katika kikao hicho basi ana dhambi kutoka kwa Allah, na anayelala sehemu yoyote ile kisha asimtaje Allah wakati wa kuinuka sehemu hiyo basi ana dhambi kwa Allah)) [Abu Daawuud]

 وقال صلى الله عليه وسلم (( ما من قوم يقومون من مجلس لا يذكرون الله فيه إلا قاموا عن مثل جيفة حمار وكان لهم حسرة)) ابو داود و أحمد

Na amesema Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Hapana watu wowote wale wanaosimama katika kikao walichokaa, kisha wasimtaje Allah ila watakuwa wanasimama kama  mzoga wa punda, na watakuja juta kwa kutomtaja Allah)) [Abu Daawuud na Ahmad]

Bonyeza hapa upate Kitabu cha Hiswnul-Muslimi kilichokusanya aina nyingi za Dhikru-Allah za kila nyakati, kila hali na popote ulipo:

 Du'aa Na Adhkhaar (Kitacbu Cha Hiswnul-Muslim)

 

Baadhi ya Dhikru-Allah zenye thawabu nyingi:

Dhikru-Allah hizi unaweza kuzisema huku ukiwa unafanya kazi zako; unapoelekea kazini, unapopika jikoni au kufanya kazi zako nyingine za nyumba, wakati wowote mahali popote.

Milioni za thawabu

 

 سُبْحـانَ اللهِ وَبِحَمْـدِهِ عَدَدَ خَلْـقِه ، وَرِضـا نَفْسِـه ، وَزِنََـةَ عَـرْشِـه ، وَمِـدادَ كَلِمـاتِـه

Subhaana-Llaahi wa Bihamdihi 'Adada Khalqihi wa Ridhwaa Nafsihi, wa Ziynata 'Arshihi wa Midaada Kalimaatih [Taja mara tatu] [Muslim]

“Ametakasika Allah  na Sifa njema zote ni Zake, kwa hisabu ya viumbe Vyake, na Radhi Rake, na uzito wa 'Arshi Yake, na wino wa maneno Yake “

Mfano mmoja tu wa thawabu hizo ni idadi ya viumbe vya Allah. Je viumbe vingapi viliokuweko duniani tokea kuumbwa Adam hadi siku ya mwisho;  Malaika, Binaadamu, Majini, wanyama wakubwa na wadogo, wa nchi kavu, baharini, angani, miti na mimea ya kila aina ulimwenguni kote, je ni thawabu ngapi hizo mtu atazichuma kutaja maneno hayo tu ambayo hata hayamchukui zaidi ya dakika moja?

Maneno mawili yenye kupendwa sana na Allah   

 

قال النبي صلّى الله عليه وسلّم :  ))كلمتان خفيفتان على اللسان ثقيلتان في الميزان حبيبتان إلى الرحمن : سبحان الله وبحمده ، سبحان الله العظيم  ((رواه البخاري ومسلم

 

Amesema Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((Maneno mawili ni mepesi mno juu ya ulimi, mazito mno katika mizani, yanapendeza mno mbele ya Ar-Rahmaan (Mwenye kurehemu) nayo ni:

سُبْحانَ اللهِ وَبِحَمْدِهِ  سُبْحَانَ اللهِ العَظِيمِ  

Subhaana-Llahi Wa-Bihamdihi Subhaana-Llahi-l-'Adhwiym)) [Ametakasika Allah na sifa njema zote ni zake, Ametakasika Allah Aliye Mtukufu] [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Thawabu za aina mbali mbali

 Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakaye sema:

 لا إِلهَ إِلَّا اللهُ وَحْدَهُ لا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ المُلْكُ وَلَهُ الحَمْد، وهُوَ عَلى كُلِّ شَيءٍ قَديرٌ

 Laa Ilaaha Illa Allaah Wah-dahu Laa Shariyka Lahu, Lahul-Mulku Wa-Lahul-hamdu Wa Huwa 'Alaa Kulli Shay-in qadiyr

"Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Allah, hali ya kuwa peke yake Hana mshirika, ni Wake Ufalme na ni Zake kila sifa njema, na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza" (mara kumi, ni kama  thawabu za mtu  aliyeacha huru nafsi nne katika wana wa Ismaa'iyl)) [al-Bukhaariy na Muslim]

Na katika riwaya nyingine: ((Atakayesema mara 100 atapata thawabu za kuacha huru nafsi kumi, ataandikiwa mema mia, atafutiwa maovu mia, itakuwa ni kinga kutokana na shaytwaan na atakuwa ni mja bora kabisa siku hiyo ila atokee atakayesema zaidi ya aliyoyasema)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Dhikru ya Allah iliyo bora kabisa

 عـَن جـَابر رضيَ الله ُ عنه قال : سـَمعتُ رسولُ الله صلى الله علـَيـْه وسـَلم ((أَفْضـَلُ الذّكرِ : لا إلهَ إِلا الله))  رواه الترمذي  

Kutoka kwa Jaabir (Radhiy Allahu 'anhu) ambaye amesema: "Nimemsikia Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Dhikr iliyo bora kabisa ni Laa ilaaha Illa-Allah)) "Hapana mola apasae kuabudiwa kwahaki ila ni Mwenyezi Mungu"  [At-Trimidhy]

 

Maneno manne bora kabisa kwa Allah

 قال صلى الله عيه وسلم:  ((أحب الكلام إلى الله أربعٌ : سبحان الله ، والحمد لله ، ولا إله إلا الله ، والله أكبر ، لا يضرك بأيهنَّ بدأت))  مسلم

 Amesema Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((Maneno Anayoyapenda Allah kuliko yote ni manne; 'Subhaana Allah, wal-Hamduli-Llaah, wa laa ilaaha illa-Allah, wa Allahu-Akbar' Si vibaya kuanza kwa lolote katika haya)) [Muslim]

Kuswaliwa mara kumi na Allah

Na tusisahau pia kumswalia kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwani ni fadhila kubwa:

 عنْ عبد اللَّه بن عمرو بن العاص ، رضي اللَّه عنْهُمَا أنَّهُ سمِع رسُول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يقُولُ : (( من صلَّى عليَّ صلاَةً ، صلَّى اللَّه علَيّهِ بِهَا عشْراً))   رواهُ مسلم

Imetoka kwa 'Abdullah ibn 'Amru ibn Al'Aasw (Radhiya Allahu 'anhumaa) kwamba kamsikia Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anasema,  (Atakayeniswalia Swalah moja Allaah Atamswalia mara kumi)) [Muslim]

Ametufundisha Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) namna ya kumswalia kama katika Hadiyth ifuatayo:

 عنْ أبي مسْعُود الْبدْريِّ ، رضي اللَّه عنْهُ ، قالَ : أَتاناَ رسُولُ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم ، وَنَحْنُ في مَجْلِس سعد بنِ عُبَادَةَ رضي اللَّه عنهُ ، فقالَ لهُ بَشِيرُ بْنُ سعدٍ : أمرَنَا اللَّه أنْ نُصلِّي علَيْكَ يا رسولَ اللَّهِ ، فَكَيْفَ نُصَّلي علَيْكَ ؟ فَسكَتَ رسولُ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم ، حتى تَمنَّيْنَا أنَّه لمْ يَسْأَلْهُ ، ثمَّ قال رسولُ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم  (( قولُوا : اللَّهمَّ صلِّ عَلى مُحَمَّدٍ ، وَعَلى آلِ مُحمَّدٍ ، كما صليْتَ على آل إبْراهِيم ، وَبارِكْ عَلى مُحَمَّد ، وعَلى آلِ مُحمَّد ، كما بَاركْتَ عَلى آل إبْراهِيم ، إنكَ حمِيدٌ مجِيدٌ ، والسلام كما قد عَلِمتم )) رواهُ مسلمٌ

Imetoka kwa Abu Mas'uud Al-Badriy (Radhiya Allahu 'anhu) ambaye amesema: Alitujia Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  na sisi tulikuwa katika majlis (ukumbi) wa Sa'ad ibn 'Ubaadah (Radhiya Allahu 'anhu), Bashiyr ibn Sa'ad akamwambia, Allaah Ametuamrisha tukuswalie ewe Mjumbe wa Allaah, je, Vipi tukuswalie? Akanyamaza Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mpaka tukatamani kwamba asingelimuuliza.  Kisha akasema Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Semeni : Allaahumma Swalli 'alaa Muhammadin wa 'alaa aali Muhammadin kamaa Swallayta 'alaa aali Ibraahiym, wa Baarik 'alaa Muhammadin wa 'alaa aali Muhammadin kama Baarakta 'alaa aali Ibrahiym Innaka Hamiydum-Majiyd.  Na salamu kama mlivyofundishwa)) [ Musli

 

************