Amefiwa Na Ndugu Yake Akiwa Mbali, Anaweza Kumswalia Ghayb?

SWALI:

  

Ndugu yangu kafa lakini mimi sinipo naweza kumsaliya mahali nilipo?


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu kumswaliya nduguyo aliyekufa sehemu mbali nawe.

Hakika ni kuwa mtu hafai kumswalia yeyote yule aliyekufa mbali ikiwa maiti ataswaliwa na Waislamu waliopo huko. Itafaa kwako kumswalia hapo ulipo ikiwa huko alikofia nduguyo hakuna Waislamu na hivyo hakuswaliwa. 

 

Kwa sasa ni vigumu kupata sehemu ambayo hakuna Waislamu. Kitu ambacho unaweza kufanya ni kumuombea du’aa kwa Allaah Aliyetukuka ili Amsamehe na Amuweke pema.

 

Soma jibu kuhusiana na swali kama lako katika kiungo kifuatacho:

 

Swalah Ya Ghayb (Kumswalia Swalah Maiti Aliye Mbali)

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share