Sajda Ya Kisomo - Kusujudu Wakati Wa Makruuh Inafaa Unaposoma Qur-aan?

SWALI:

 

Assalam alekum

 

Tunashukuru kwa kutelimisha Mwenyezi Mungu awalipe mema awalinde na shari. Swali langu ni kuhusu kusujudu baada ya kusoma aya yenye alama ya kusujudu. Nnaposoma Qur’aani baada ya sala ya alfajiri ambako ni wakati unaochukiza kusali hadi litoke jua na nikapitia alama hiyo, je nisujudu au nisisujudu?

 

Nitashukuru kupata jibu.


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu wakati wa kusujudu sijdah ya kisomo. Hakika sijdah ya kisomo unaweza kusujudu wakati wowote kwani sijdah hiyo imeegemezewa kitendo fulani kinapofanywa. Hii ni kama Sijda ya kushukuru au Sunnah ya kuuamkia Msikiti (Tahiyyatul Masjid) au ya Sunnah ya wudhuu ambayo unaweza kuitekeleza wakati wowote ule hata kama ni wakati wa Makruuh.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share