Tafauti Kati Ya Aayah Zilizokuwa Zikishuka Makkah Na Zilozoshuka Madiynah

SWALI:

 

ASSALAM ALEYKUM.KILA SIFA NJEMA ANASTAHIKI MOLA WA VIUMBE VYOTE ALLAH TABARAKA WATAALA. NAOMBA KUPATA UFAFANUZI WA TOFAUTI KATI YA AYA ZILIZOKUA ZIKISHUKA MADINAH NA AYA ZILIZOKUA ZIKISHUKA MAKKAH ZILIKUA NA TOFAUTI GANI.

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu tofauti baina Aayah za Makkah na Madiynah.

Tofauti kubwa inayoonekana baina ya Aayah zilizoteremka sehemu hizo mbili tofauti ni:

 

1.   Aayah za Surah za Makkah ni za kujenga Imani na umuhimu wake Makkah lakini Madiynah ikawa ni shari’ah na utendaji kazi wake.

 

2.   Visa vya Ummah iliyopita katika Aayah za Makkah ilhali Aayah za Madiynah ni kuhusiana na ‘Ibaadah.

 

3.   Aayah na Surah za Makkah ni fupi ilhali za Madiynah zilikuwa ni ndefu.

 

4.   Kubainishwa halali na haramu katika kipindi cha Madiynah ilhali Makkah hakukuwa na Aayah aina hizo.

 

5.   Aayah kuhusiana na shirki na ukafiri huko Makkah ilhali Madiynah ni Aayah kuhusiana na waliopewa Kitabu.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share