Kuzini Ndani Ndoa Nini Hukmu Yake?

 

SWALI:

Assalaam alaykum.

Kwanza natoa shukran zote kwa kuwepo website hii na pia nawapa shukran nyote munaoa tusaidia tuliyokua hatuyajui nawatakia kila la kheir shukran

Swali langu ni.

Naomba kuuliza kua mke akiwa amezini na akamtamkia mume wake kua amefanya hicho kitendo itakua ameachika kwa kufanya hicho kitendo au mpaka mume ampe talaka ndioa kaachika. Na pia itakua mke keshaharamika kwa mume wake? Au, naomba majibu inshaalla mapema ikiwezekana ameen

 


 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukran kwa ndugu yetu kwa swali lako hili. Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atuepushe na magonjwa haya ya zinaa na maasiya mengineyo. Ieleweke kuwa mke ana madhambi kwa kitendo hicho chake cha kuzini. Kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema: “Na wale wasio mwomba mungu mwengine pamoja na Allaah, wala hawaui nafsi aliyo iharimisha Allaah isipokuwa kwa haki, wala hawazini - na atakayefanya hayo atapata madhara, Atazidishiwa adhabu Siku ya Qiyaamah, na atadumu humo kwa kufedheheka” (25: 68 – 69).

Lau kama kungelikuweko Dola ya Kiislamu ambayo ingelitimiza adhabu ya kumpa mwenye kuzini, basi bila shaka maasi haya yangeliogopewa na kila Muislamu. Hivyo bila shaka hakuna yeyote ambaye angelithubutu kufanya maasi haya.

Hivyo ingelibidi kwa kukiri kwake kuwa kazini, hukumu yake ingekuwa ni kuuliwa kama ndio Hadd (Adhabu) yake hapa duniani, na kesho Akhera atakuwa amesamehewa. Hadd yake ni kupigwa mawe mpaka kufa.

Mke kama huyu bado hajaachika mpaka mume wake ampatie talaka.

Mke huyo bado ni mke wa mtu na ikiwa mume atamsamehe kwa kule kutaka msamaha kwake basi ndoa yao itabakia vile vile. Na lau mume ataona kuwa hataweza kubaki naye basi atampatia talaka naye atakuwa ni mwenye kukaa eda lakini kwa sababu ya kosa lake hatakaa kwa mumewe. Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema:

Ewe Nabii! Mtakapo wapa talaka wanawake, basi wapeni talaka katika wakati wa eda zao. Na fanyeni hisabu ya eda. Na mcheni Allaah, Mola wenu  Msiwatoe katika nyumba zao, wala wasitoke wenyewe, ila wakifanya jambo la uchafu ulio wazi. Hiyo ndiyo mipaka ya Allaah, msiikiuke. Na mwenye kuikiuka mipaka ya Allaah, basi amejidhulumu nafsi yake. Hujui; labda Allaah ataleta jambo jengine baada ya haya” (65: 1).

Maelezo ya maana ya Aayah hii kama alivyoelezea Shaykh 'Abdallah Swaalih Al-Farsy katika 'Qur-aan Takatifu'.

Surah hii inataja habari nyingi zilizokhusiana na talaka.  Talaka kama alivyosema Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) dhahiri shahiri katika Hadithi zake.

Talaka imewekwa itokee itakapotokea dharura iwe kama dawa si chakula. Na wenye kuoana  wa kikwetu wameifanya talaka ndicho chakula cha ndoa, lazima kutokea kwa kila mwenye kuoa.

Basi hapa zinatajwa kidogo sharti za kuacha:

i)   Fatwalliquu-hunna li'ddatihinna

Na Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alifasiri tamko hili kwa kuwa hapana ruhusa kumuacha mwanamke anapokuwa yumo:

     a)   Miezini au

b)   Katika tahara lakini wampeta kuonana katika tahara hiyo.

Mwanamume akipandwa na hamaki akataka kumuacha mkewe hana ruhusu kumuambia: "Nimekuacha". Lazima amuulize kwanza yumo miezini (katika hedhi) au safi. Akiwa yumo miezini hana ruhusa  kumuacha. Akimuacha atapata dhambi. Wala mtu asiyaonee ajabu haya. Haya yanatajwa katika vitabu vyote vya Fiqhi, vikubwa na vidogo hata katika kijitabu kidogo hiki cha Safina. 

Kama yuko miezini, basi itampasa angojee mpaka aingie katika tahara ndipo amuache. Na Wakati huo hawataachana tena kwani shetani atakuwa kisha kuruka zamani. 

Na ikiwa yumo katika tahara waliyoingiliana, basi lazima angojee mpaka tahara hiyo ishe, aingie miezini, ishe ada yake ya mwezi aingie katika tahara.  Kabla ya kuingiliana amuache. Wala hawataachana vile vile kwani shetani atakuwa ameruka zamani.

ii)          Laa tukhrijuuhunna min buyuutihinna

 

Msiwatoe katika majumba yao. Yaani ukimuacha huna ruhusa kumtoa nyumbani. Asalie katika nyumba hiyo  hiyo kwa kula na kupewa nguo mpaka eda yake ishe, kama ilivyo vile katika Aayah ya 6 na ya 7 za Surah hii hii.

 

Mume ndiye ajitenge chumba mbali na choo mbali. Ikiwa hapana nafasi, basi atoke yeye mume akatafute nyumba nyingine ya kukaa mpaka ishe eda ndiyo bibi atokea na achukue vyake. Na wala hatawahi kutoka kwani pengine watakuwa wamekwisha kurejeana. Inataka awe shetani mkubwa huyo hata muda wa miezi mitatu kuwa bado tu hajawatoka! Basi hii ndio Laalla-Llaaha Yuhdithu Ba'ada Dhaalika Amra.

iii)   Wa-ahswul-'iddah

       Wadhibiti siku za eda ili warejeane kabla ya kumalizika.

Na Allah Anajua zaidi

     

 

Share