080 - 'Abasa

 

 

 

عَبَسَ

‘Abasa: 080

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

عَبَسَ وَتَوَلَّىٰ ﴿١﴾

1. Alikunja kipaji na akageuka.

 

 

أَن جَاءَهُ الْأَعْمَىٰ ﴿٢﴾

2. Kwa kuwa kipofu alimjia.

 

 

وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّهُ يَزَّكَّىٰ ﴿٣﴾

3. Na nini kitakachokujulisha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) huenda akatakasika?

 

 

أَوْ يَذَّكَّرُ فَتَنفَعَهُ الذِّكْرَىٰ ﴿٤﴾

4. Au atawaidhika na yamfae mawaidha?

 

 

أَمَّا مَنِ اسْتَغْنَىٰ ﴿٥﴾

5. Ama yule ajionaye amejitosheleza.

 

 

فَأَنتَ لَهُ تَصَدَّىٰ ﴿٦﴾

6. Wewe ndio unamgeukia kumshughulikia!

 

 

وَمَا عَلَيْكَ أَلَّا يَزَّكَّىٰ ﴿٧﴾

7. Na si juu yako asipotakasika.

 

 

 

وَأَمَّا مَن جَاءَكَ يَسْعَىٰ ﴿٨﴾

8. Ama yule aliyekujia kwa shime na hima.

 

 

وَهُوَ يَخْشَىٰ ﴿٩﴾

9. Naye anakhofu.

 

 

فَأَنتَ عَنْهُ تَلَهَّىٰ ﴿١٠﴾

10. Basi wewe unampuuza!

 

 

كَلَّا إِنَّهَا تَذْكِرَةٌ ﴿١١﴾

11. Laa hasha! Hakika hizi (Aayah) ni mawaidha.

 

 

فَمَن شَاءَ ذَكَرَهُ ﴿١٢﴾

12. Basi atakaye na awaidhike nayo (Qur-aan).

 

 

فِي صُحُفٍ مُّكَرَّمَةٍ ﴿١٣﴾

13.  Yamo hayo katika Sahifa zenye kuadhimishwa.

 

 

مَّرْفُوعَةٍ مُّطَهَّرَةٍ ﴿١٤﴾

14. Zimetukuzwa na zimetakaswa.

 

 

بِأَيْدِي سَفَرَةٍ ﴿١٥﴾

15. Katika mikono ya Malaika waandishi.

 

 

 

كِرَامٍ بَرَرَةٍ ﴿١٦﴾

16. Watukufu, watiifu.

 

 

 

قُتِلَ الْإِنسَانُ مَا أَكْفَرَهُ ﴿١٧﴾

17. Amelaaniwa na kuangamia binaadamu, ukafiri ulioje alionao?

 

 

مِنْ أَيِّ شَيْءٍ خَلَقَهُ ﴿١٨﴾

18. Kutoka kitu gani (Allaah) Amemuumba?

 

 

مِن نُّطْفَةٍ خَلَقَهُ فَقَدَّرَهُ ﴿١٩﴾

19. Kutoka tone la manii, Amemuumba, Akamkadiria.

 

 

ثُمَّ السَّبِيلَ يَسَّرَهُ ﴿٢٠﴾

20. Kisha Akamuwepesishia njia.

 

 

ثُمَّ أَمَاتَهُ فَأَقْبَرَهُ ﴿٢١﴾

21. Kisha Akamfisha, na Akampa takrima ya kuzikwa.

 

 

 

ثُمَّ إِذَا شَاءَ أَنشَرَهُ ﴿٢٢﴾

22. Kisha Atakapotaka, Atamfufua.

 

 

كَلَّا لَمَّا يَقْضِ مَا أَمَرَهُ ﴿٢٣﴾

23. Laa hasha! Hakutimiza bado Aliyomuamuru (Allaah).

 

 

 

فَلْيَنظُرِ الْإِنسَانُ إِلَىٰ طَعَامِهِ ﴿٢٤﴾

24. Basi atazame binaadamu chakula chake.

 

 

أَنَّا صَبَبْنَا الْمَاءَ صَبًّا ﴿٢٥﴾

25. Kwamba Sisi Tumemimina maji kwa uneemefu.

 

 

ثُمَّ شَقَقْنَا الْأَرْضَ شَقًّا ﴿٢٦﴾

26. Kisha Tukaipasua ardhi ikafunguka (kwa mimea).

 

 

فَأَنبَتْنَا فِيهَا حَبًّا ﴿٢٧﴾

27. Tukaotesha humo nafaka.

 

 

وَعِنَبًا وَقَضْبًا ﴿٢٨﴾

28. Na mizabibu na mimea ya mboga (ikatwayo ikamea tena).

 

 

وَزَيْتُونًا وَنَخْلًا ﴿٢٩﴾

29. Na mizaituni na mitende.

 

 

وَحَدَائِقَ غُلْبًا ﴿٣٠﴾

30. Na mabustani yaliyositawi na kusongamana.

 

 

وَفَاكِهَةً وَأَبًّا ﴿٣١﴾

31. Na matunda na majani ya malisho ya wanyama.

 

 

مَّتَاعًا لَّكُمْ وَلِأَنْعَامِكُمْ ﴿٣٢﴾

32. Yakiwa ni manufaa kwenu na kwa wanyama wenu wa mifugo.

 

 

فَإِذَا جَاءَتِ الصَّاخَّةُ ﴿٣٣﴾

33. Basi utakapokuja ukelele mkali wa kuvuruga masikio.

 

 

 

يَوْمَ يَفِرُّ الْمَرْءُ مِنْ أَخِيهِ ﴿٣٤﴾

34. Siku mtu atakapomkimbia ndugu yake.

 

 

وَأُمِّهِ وَأَبِيهِ ﴿٣٥﴾

35. Na mama yake na baba yake.

 

 

وَصَاحِبَتِهِ وَبَنِيهِ ﴿٣٦﴾

36. Na mkewe na wanawe.

 

 

لِكُلِّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ يَوْمَئِذٍ شَأْنٌ يُغْنِيهِ ﴿٣٧﴾

37. Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na hali yake ya kumtosha mwenyewe.

 

 

 

وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ مُّسْفِرَةٌ ﴿٣٨﴾

38.  Ziko nyuso siku hiyo zitanawiri.

 

 

ضَاحِكَةٌ مُّسْتَبْشِرَةٌ ﴿٣٩﴾

39. Zikicheka na kufurahika.

 

 

وَوُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ عَلَيْهَا غَبَرَةٌ ﴿٤٠﴾

40. Na ziko nyuso siku hiyo zitakuwa na vumbi juu yake.

 

 

تَرْهَقُهَا قَتَرَةٌ ﴿٤١﴾

41. Zitafunikwa na giza totoro.

 

 

أُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَفَرَةُ الْفَجَرَةُ ﴿٤٢﴾

42. Hao ndio makafiri waovu.

 

 

 

Share