080-Asbaabun-Nuzuwl: 'Abasa Aayah 1-10: عَبَسَ وَتَوَلَّىٰ

 

 

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

080-'Abasa

 

عَبَسَ وَتَوَلَّىٰ ﴿١﴾

1. Alikunja kipaji na akageuka.

 

أَن جَاءَهُ الْأَعْمَىٰ ﴿٢﴾

2. Alipomjia kipofu.

 

وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّهُ يَزَّكَّىٰ ﴿٣﴾

3. Na nini kitakachokujulisha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) huenda akatakasika?

 

أَوْ يَذَّكَّرُ فَتَنفَعَهُ الذِّكْرَىٰ ﴿٤﴾

4. Au atawaidhika na yamfae mawaidha?

 

أَمَّا مَنِ اسْتَغْنَىٰ ﴿٥﴾

5. Ama yule ajionaye amejitosheleza.

 

فَأَنتَ لَهُ تَصَدَّىٰ ﴿٦﴾

6. Nawe unamgeukia kumshughulikia.

 

وَمَا عَلَيْكَ أَلَّا يَزَّكَّىٰ ﴿٧﴾

7. Na si juu yako asipotakasika.

 

وَأَمَّا مَن جَاءَكَ يَسْعَىٰ ﴿٨﴾

8. Ama yule aliyekujia kwa kukimbilia.

 

وَهُوَ يَخْشَىٰ ﴿٩﴾

9. Naye anakhofu.

 

فَأَنتَ عَنْهُ تَلَهَّىٰ ﴿١٠﴾

10. Basi wewe unampuuza.

 

 

حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ يَحْيَى بْنِ سَعِيدٍ الأُمَوِيُّ، حَدَّثَنِي أَبِي قَالَ، هَذَا مَا عَرَضْنَا عَلَى هِشَامِ بْنِ عُرْوَةَ عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ أُنْزِلَ ‏:‏((عبَسَ وَتَوَلَّى))‏ فِي ابْنِ أُمِّ مَكْتُومٍ الأَعْمَى أَتَى رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَجَعَلَ يَقُولُ يَا رَسُولَ اللَّهِ أَرْشِدْنِي وَعِنْدَ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم رَجُلٌ مِنْ عُظَمَاءِ الْمُشْرِكِينَ فَجَعَلَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يُعْرِضُ عَنْهُ وَيُقْبِلُ عَلَى الآخَرِ وَيَقُولُ أَتَرَى بِمَا أَقُولُ بَأْسًا فَيُقَالُ لاَ ‏.‏ فَفِي هَذَا أُنْزِلَ

 

Ametuhadithia said bin Yahyya bin Sa’iyd Al-Amawiy amesema amenihadithia baba yangu amesema: Hili tulimtajia Hishaam bin ‘Urwat kutoka kwa baba yake kutoka kwa ‘Aaishah imeteremka:

عَبَسَ وَتَوَلَّىٰ ﴿١﴾

1. Alikunja kipaji na akageuka.

 

Kwa ibn Ummi Maktuwm aliyekuwa kipofu alikuwa kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) mara akaingia mmoja wa watu wakubwa miongoni mwa washirikina, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akawa anamuelezea Yule mshirikina kuhusiana naye, na anamuelekea akisema:  “Je, ninalolisema unaliona baya”  kwa ajili hii ikateremka.

 

[Hadiyth hii ni Hasan Ghariyb na wengine wamepokea Hadiyth hii kutoka kwa Hishaam bin ‘Urwah kutoka kwa baba yakekuwa amesema kuwa:

 

Alikunja kipaji na akageuka”

 

Imeteremka kwa Ibn Ummi Maktuwm na hakumtaja ‘Aaishah. [At-Tirmidhiy – Kitaab At-Tafiyr Al-Qur-aan kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم

 

Wametaja wafasiri wengi kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) siku moja alikuwa akizungumza na viongozi wa ma-Quraysh na alikuwa ametaraji katika kusilimu kwa baadhi ya viongozi hao. Wakati akiwa katika mazungumzo nao, ghafla akatokezea Ibnu Ummi Maktuwm ambaye alikuwa miongoni mwa watu waliosilimu hapo kabla akawa anamuuliza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu jambo na huku akishikilia hilo la muhimu. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alitaraji  kuwa atamuongoa kiongozi huyo wa Quraysh. Akamwambia ibn Maktuwm asubiri ili amalize maongezi nao. Akakunja uso na akampa mgongo na akaelekea kwa yule mwingine hapo Allaah Akateremsha:

عَبَسَ وَتَوَلَّىٰ ﴿١﴾

1. Alikunja kipaji na akageuka.

أَن جَاءَهُ الْأَعْمَىٰ ﴿٢﴾

2. Alipomjia kipofu.

 

 

 

Share