079 - An-Naazi'aat
النَّازِعَات
An-Naazi’aat: 079
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
وَالنَّازِعَاتِ غَرْقًا ﴿١﴾
1. Naapa kwa wanaong’oa (roho) kwa nguvu.
وَالنَّاشِطَاتِ نَشْطًا ﴿٢﴾
2. Na Naapa kwa wanaotoa (roho) kwa upole.
وَالسَّابِحَاتِ سَبْحًا ﴿٣﴾
3. Na Naapa kwa wanaoogelea kwa kupanda na kushuka (katika anga).
فَالسَّابِقَاتِ سَبْقًا ﴿٤﴾
4. Kisha Naapa kwa wenye kutangulia mbele kwa kushindana.
فَالْمُدَبِّرَاتِ أَمْرًا ﴿٥﴾
5. Kisha Naapa kwa wenye kuendesha kila jambo.
يَوْمَ تَرْجُفُ الرَّاجِفَةُ ﴿٦﴾
6. Siku kitakapotetemeka chenye kutetemesha (mpulizo wa awali).
تَتْبَعُهَا الرَّادِفَةُ ﴿٧﴾
7. Kifuatiliwe na cha pili yake (mpulizo wa pili).
قُلُوبٌ يَوْمَئِذٍ وَاجِفَةٌ ﴿٨﴾
8. Nyoyo siku hiyo zitapuma kwa nguvu kutokana na khofu.
أَبْصَارُهَا خَاشِعَةٌ ﴿٩﴾
9. Macho yake yatainama chini.
يَقُولُونَ أَإِنَّا لَمَرْدُودُونَ فِي الْحَافِرَةِ ﴿١٠﴾
10. Wanasema (sasa): Je, hivi sisi tutarudishwa katika hali ya asili ya uhai?
أَإِذَا كُنَّا عِظَامًا نَّخِرَةً ﴿١١﴾
11. Je, hata tukiwa ni mifupa iliyosagika na kuoza?
قَالُوا تِلْكَ إِذًا كَرَّةٌ خَاسِرَةٌ ﴿١٢﴾
12. Hayo basi ni marejeo ya khasara.
فَإِنَّمَا هِيَ زَجْرَةٌ وَاحِدَةٌ ﴿١٣﴾
13. Basi hakika huo ni ukelele mmoja tu wa kuogofya.
فَإِذَا هُم بِالسَّاهِرَةِ ﴿١٤﴾
14. Tahamaki hao wamekusanyika uwandani wakiwa macho baada ya kufa.
هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ مُوسَىٰ ﴿١٥﴾
15. Je, imekufikia hadithi ya Muwsaa?
إِذْ نَادَاهُ رَبُّهُ بِالْوَادِ الْمُقَدَّسِ طُوًى ﴿١٦﴾
16. Pale Rabb wake Alipomuita kwenye Bonde Takatifu la Tuwaa.
اذْهَبْ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ إِنَّهُ طَغَىٰ ﴿١٧﴾
17. (Akamwambia): Nenda kwa Firawni, hakika yeye amepindukia mipaka ya kuasi.
فَقُلْ هَل لَّكَ إِلَىٰ أَن تَزَكَّىٰ ﴿١٨﴾
18. Umwambie: Je, unataka utakasike?
وَأَهْدِيَكَ إِلَىٰ رَبِّكَ فَتَخْشَىٰ ﴿١٩﴾
19. Na nikuongoze kwa Rabb wako umuogope?
فَأَرَاهُ الْآيَةَ الْكُبْرَىٰ ﴿٢٠﴾
20. Basi akamuonyesha ishara kubwa kabisa.
فَكَذَّبَ وَعَصَىٰ ﴿٢١﴾
21. Lakini akakadhibisha, na akaasi.
ثُمَّ أَدْبَرَ يَسْعَىٰ ﴿٢٢﴾
22. Kisha akageuka nyuma na akapania kufanya juhudi (za kukanusha haki).
فَحَشَرَ فَنَادَىٰ ﴿٢٣﴾
23. Akakusanya watu kisha akanadi.
فَقَالَ أَنَا رَبُّكُمُ الْأَعْلَىٰ ﴿٢٤﴾
24. Akasema: Mimi ni mola wenu mkuu.
فَأَخَذَهُ اللَّـهُ نَكَالَ الْآخِرَةِ وَالْأُولَىٰ ﴿٢٥﴾
25. Basi Allaah Alimchukuwa kwa adhabu ya tahadharisho na fundisho ya Aakhirah (ya moto) na ya mwanzo ya (duniani ya kugharikishwa).
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبْرَةً لِّمَن يَخْشَىٰ ﴿٢٦﴾
26. Hakika katika hayo bila shaka kuna funzo kwa yule anayeogopa.
أَأَنتُمْ أَشَدُّ خَلْقًا أَمِ السَّمَاءُۚ بَنَاهَا ﴿٢٧﴾
27. Je, kuumbwa nyinyi ndio vigumu zaidi au mbingu? Kaijenga (Yeye)
رَفَعَ سَمْكَهَا فَسَوَّاهَا ﴿٢٨﴾
28. Amenyanyua kimo chake, kisha Akazisawazisha sawasawa.
وَأَغْطَشَ لَيْلَهَا وَأَخْرَجَ ضُحَاهَا ﴿٢٩﴾
29. Na Akatia kiza usiku wake, na Akatokezesha mwanga wa mchana wake.
وَالْأَرْضَ بَعْدَ ذَٰلِكَ دَحَاهَا ﴿٣٠﴾
30. Na ardhi baada ya hayo Akaitandaza.
أَخْرَجَ مِنْهَا مَاءَهَا وَمَرْعَاهَا ﴿٣١﴾
31. Akatoa humo maji yake na malisho yake.
وَالْجِبَالَ أَرْسَاهَا ﴿٣٢﴾
32. Na milima Akaikita imara.
مَتَاعًا لَّكُمْ وَلِأَنْعَامِكُمْ ﴿٣٣﴾
33. Kwa ajili ya manufaa kwenu na kwa wanyama wenu wa mifugo.
فَإِذَا جَاءَتِ الطَّامَّةُ الْكُبْرَىٰ ﴿٣٤﴾
34. Basi itakapokuja balaa kubwa kabisa ya kuvuka mpaka.
يَوْمَ يَتَذَكَّرُ الْإِنسَانُ مَا سَعَىٰ ﴿٣٥﴾
35. Siku binaadamu atakapokumbuka yale aliyoyakimbilia kwa juhudi.
وَبُرِّزَتِ الْجَحِيمُ لِمَن يَرَىٰ ﴿٣٦﴾
36. Na moto wa jahiym (uwakao vikali mno) utakapodhihirishwa wazi kwa aonaye.
فَأَمَّا مَن طَغَىٰ ﴿٣٧﴾
37. Basi yule aliyepindukia mipaka kuasi.
وَآثَرَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا ﴿٣٨﴾
38. Na akahiari uhai wa dunia.
فَإِنَّ الْجَحِيمَ هِيَ الْمَأْوَىٰ ﴿٣٩﴾
39. Basi hakika jahiym (moto uwakao vikali mno) ndio makaazi yake.
وَأَمَّا مَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِ وَنَهَى النَّفْسَ عَنِ الْهَوَىٰ ﴿٤٠﴾
40. Ama yule aliyekhofu kisimamo mbele ya Rabb wake, na akaikataza nafsi yake na hawaa.
فَإِنَّ الْجَنَّةَ هِيَ الْمَأْوَىٰ ﴿٤١﴾
41. Basi hakika Jannah ndio makaazi yake.
يَسْأَلُونَكَ عَنِ السَّاعَةِ أَيَّانَ مُرْسَاهَا ﴿٤٢﴾
42. Wanakuuliza (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu Saa lini kufika kwake?
[3]
فِيمَ أَنتَ مِن ذِكْرَاهَا ﴿٤٣﴾
43. Huna ujuzi wewe hata utaje lolote.
إِلَىٰ رَبِّكَ مُنتَهَاهَا ﴿٤٤﴾
44. Kwa Rabb wako ndio kuishia kwake (ujuzi wake).
إِنَّمَا أَنتَ مُنذِرُ مَن يَخْشَاهَا ﴿٤٥﴾
45. Hakika wewe ni muonyaji wa yule anayeikhofu.
كَأَنَّهُمْ يَوْمَ يَرَوْنَهَا لَمْ يَلْبَثُوا إِلَّا عَشِيَّةً أَوْ ضُحَاهَا ﴿٤٦﴾
46. Siku watakapoiona, watakuwa kama kwamba hawakubaki (duniani) isipokuwa jioni moja au mchana wake.
