082 - Al-Infitwaar

 

 

 

الإِنْفِطَار

Al-Infitwaar: 082

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

إِذَا السَّمَاءُ انفَطَرَتْ ﴿١﴾

1. Mbingu itakapopasuka.

 

 

وَإِذَا الْكَوَاكِبُ انتَثَرَتْ ﴿٢﴾

2. Na sayari zitakapoanguka na kutawanyika.

 

 

وَإِذَا الْبِحَارُ فُجِّرَتْ ﴿٣﴾

3. Na bahari zitakapopasuliwa.

 

 

وَإِذَا الْقُبُورُ بُعْثِرَتْ ﴿٤﴾

4. Na makaburi yatakapopinduliwa chini juu na kufichuliwa.

 

 

عَلِمَتْ نَفْسٌ مَّا قَدَّمَتْ وَأَخَّرَتْ ﴿٥﴾

5. Nafsi hapo itajua yale iliyoyakadimisha na iliyoyaakhirisha.

 

 

يَا أَيُّهَا الْإِنسَانُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ الْكَرِيمِ ﴿٦﴾

6. Ee binaadamu! Nini kilichokughuri hata umkufuru Rabb wako Mkarimu?

 

 

الَّذِي خَلَقَكَ فَسَوَّاكَ فَعَدَلَكَ ﴿٧﴾

7. Ambaye Amekuumba, Akakusawazisha (umbo sura, viungo), na Akakulinganisha sawa.

 

 

فِي أَيِّ صُورَةٍ مَّا شَاءَ رَكَّبَكَ ﴿٨﴾

8. Katika sura Aliyotaka Akakutengeneza.

 

 

كَلَّا بَلْ تُكَذِّبُونَ بِالدِّينِ ﴿٩﴾

9. Laa hasha! Bali mnakadhibisha malipo.

 

 

وَإِنَّ عَلَيْكُمْ لَحَافِظِينَ ﴿١٠﴾

10. Na hakika juu yenu bila shaka kuna wenye kuhifadhi (na kuchunga).  

 

 

كِرَامًا كَاتِبِينَ ﴿١١﴾

11. Watukufu wanaoandika (amali).

 

 

يَعْلَمُونَ مَا تَفْعَلُونَ ﴿١٢﴾

12. Wanajua yale myafanyayo.

 

 

إِنَّ الْأَبْرَارَ لَفِي نَعِيمٍ ﴿١٣﴾

13. Hakika Al-Abraar (watendao khayraat kwa wingi) bila shaka watakuwa katika neema (taanasa, furaha n.k).

 

 

وَإِنَّ الْفُجَّارَ لَفِي جَحِيمٍ ﴿١٤﴾

14. Na hakika watendao dhambi bila shaka watakuwa katika moto uwakao vikali mno.

 

 

يَصْلَوْنَهَا يَوْمَ الدِّينِ ﴿١٥﴾

15. Watauingia waungue Siku ya malipo.

 

 

 

وَمَا هُمْ عَنْهَا بِغَائِبِينَ ﴿١٦﴾

16. Nao hawatokosa kuweko humo.

 

 

وَمَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الدِّينِ ﴿١٧﴾

17. Na nini kitakachokujulisha ni ipi Siku ya malipo?

 

 

ثُمَّ مَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الدِّينِ ﴿١٨﴾

18. Kisha nini kitakachokujulisha ni ipi Siku ya malipo?

 

 

يَوْمَ لَا تَمْلِكُ نَفْسٌ لِّنَفْسٍ شَيْئًاۖ وَالْأَمْرُ يَوْمَئِذٍ لِّلَّـهِ ﴿١٩﴾

19. Siku ambayo nafsi haitokuwa na uwezo wowote juu ya nafsi nyingine, na amri Siku hiyo ni ya Allaah Pekee.

 

 

 

 

Share