105 - Al-Fiyl

 

 

 

  الْفِيل

Al-Fiyl: 105

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

أَلَمْ تَرَ كَيْفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِأَصْحَابِ الْفِيلِ ﴿١﴾

1. Je, hukuona (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) jinsi Rabb wako Alivyowafanya watu wa tembo?

 

 

أَلَمْ يَجْعَلْ كَيْدَهُمْ فِي تَضْلِيلٍ ﴿٢﴾

2. Je, Hakujaalia hila zao kufeli na kushindwa?

 

 

وَأَرْسَلَ عَلَيْهِمْ طَيْرًا أَبَابِيلَ ﴿٣﴾

3. Na Akawatumia ndege makundi kwa makundi yafuatanayo kuwashambulia?

 

 

تَرْمِيهِم بِحِجَارَةٍ مِّن سِجِّيلٍ ﴿٤﴾

4. Wakiwarushia mawe ya udongo uliookwa motoni.

 

 

فَجَعَلَهُمْ كَعَصْفٍ مَّأْكُولٍ ﴿٥﴾

5. Akawafanya kama nyasi kavu zilizoliwa.

 

 

 

Share