272-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 272: لَّيْسَ عَلَيْكَ هُدَاهُمْ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

Al-Baqarah Aayah  272-Si juu yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuwaongoa, lakini Allaah Humwongoa Amtakaye

 

لَّيْسَ عَلَيْكَ هُدَاهُمْ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ ۗ وَمَا تُنفِقُوا مِنْ خَيْرٍ فَلِأَنفُسِكُمْ ۚ وَمَا تُنفِقُونَ إِلَّا ابْتِغَاءَ وَجْهِ اللَّـهِ ۚ وَمَا تُنفِقُوا مِنْ خَيْرٍ يُوَفَّ إِلَيْكُمْ وَأَنتُمْ لَا تُظْلَمُونَ ﴿٢٧٢﴾

272. Si juu yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuwaongoa, lakini Allaah Humwongoa Amtakaye. Na chochote cha kheri mtoacho basi ni kwa ajili ya nafsi zenu. Na hamtoi ila kutaka Wajhi wa Allaah. Na chochote mtoacho katika kheri mtalipwa kamilifu nanyi hamtodhulumiwa.

 

 Sababun-Nuzuwl:

 

Aayah hii: “Si juu yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuwaongoa…” imeteremka kuhusu Maswahaba walikuwa hawawapi hata kidogo ndugu zao wa karibu katika Washirikina, basi hapo ikateremka: Wale wanaovunja ahadi ya Allaah baada ya kuifunga Kwake na wanakata Aliyoyaamrisha Allaah kuungwa...” (2: 27). [Ibn Jariyr kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)] 

 

 

 

Share