08-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Mwenye Swawm Ya Kulipa Kutoka Ramadhwaan Iliyopita, Basi Ni Lazima Ailipe Kabla ya Ramadhwaan Nyingine Kuingia

Mwenye Swawm Ya Kulipa Kutoka Ramadhwaan Iliyopita, Basi Ni Lazima Ailipe Kabla ya Ramadhwaan Nyingine Kuingia

 

www.alhidaaya.com

 

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

 

 

"Hairuhusiwi kuahirisha ulipaji deni wa Swawm (ya Ramadhwaan iliyopita) hadi ikaingia Ramadhwaan nyingine bila udhuru (unaokubalika kishariy'ah).

Hiili ni kwa sababu ya maelezo ya mama wa Waumini 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): 'Nilikuwa na deni la Swawm ya Ramadhwaan na sikuweza kulipa ila katika Sha'baan.' [Al-Bukhaariy]

 

 

[Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 59]

Share