07-Shaykh Swaalih Al-Fawzaan: Hakuweza Swiyaam Kwa Muda Wa Miaka Minne Kwa Sababu Ya Ugonjwa

Hakuweza Swiyaam Kwa Muda Wa Miaka Minne Kwa Sababu Ya Ugonjwa

 

Shaykh Swaalih Al-Fawzaan (Hafidhwahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Mtu alifikwa na maradhi ya kudumu, na madaktari wakamnasihi asifunge. Akapona ugonjwa huo baada ya miaka minne. Afanye nini sasa baada ya Allaah kumponyesha. Alipe siku zilizopita?

 

 

JIBU:

 

Mtu yeyote aliyokuwa hakuweza Swiyaam kwa sababu ya ugonjwa, kisha akapona anatakiwa alipe Swiyaam za siku alizokuwa hakufunga kwa sababu Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

 أَيَّامًا مَّعْدُودَاتٍ ۚ فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۚ

184. (Swiyaam ni) Siku za kuhesabika. Lakini atakayekuwa mgonjwa miongoni mwenu, au yuko safarini, basi (inapaswa kulipa) idadi sawa katika masiku mengineyo

 

Kwa hiyo kama hakufunga Ramadhwaan nne zilizofuatana, kisha akapona, inampasa alipe siku zake kwa utaratibu maalum. Lakini anaweza kufunga siku mbali mbali (si moja kwa kwa moja) kutokana na uwezo wake hadi amalize na ajitoe katika jukumu hili. Haikuwajibika kwake kufunga zote pamoja bila ya kupumzika kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ  

Basi mcheni Allaah muwezavyo,  [At-Taghaabun: 16]

 

Na hivi ndivyo ilivyo kwa vile wakati wa kulipa uko mwingi.

 

 

[Shaykh Swaalih Al-Fawzaan -
Fataawaa Ramadhwaan – Mjalada 2, Uk  592, Fatwa Namba 577;
Al-Muntaqaa min Fataawaa Ash-Shaykh Swaalih Ibn Fawzaan – Mjalada  3, Uk 139]

 

 

Share