الْجُمُعَة
062-Al-Jumu’ah
062-Al-Jumu’ah: Utangulizi Wa Suwrah [1]
Alhidaaya.com [2]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
يُسَبِّحُ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ الْمَلِكِ الْقُدُّوسِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ﴿١﴾
1. Vinamsabbih Allaah Pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi, Mfalme, Ametakasika na sifa zote hasi, Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
هُوَ الَّذِي بَعَثَ فِي الْأُمِّيِّينَ رَسُولًا مِّنْهُمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِهِ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَإِن كَانُوا مِن قَبْلُ لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ﴿٢﴾
2. Yeye Ndiye Aliyepeleka Rasuli kwa wasiojua kusoma wala kuandika, atokanaye nao wenyewe, anawasomea Aayaat Zake na Anawatakasa, na Anawafunza Kitabu na Hikmah, nao (kwa hakika) walikuwa hapo kabla katika upotofu bayana.
وَآخَرِينَ مِنْهُمْ لَمَّا يَلْحَقُوا بِهِمْ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿٣﴾
3. Na wengineo ambao bado hawajakutana nao. Naye Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
ذَٰلِكَ فَضْلُ اللَّـهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ﴿٤﴾
4. Hiyo ni Fadhila ya Allaah Humpa Amtakaye, na Allaah Ni Mwenye fadhila adhimu.
مَثَلُ الَّذِينَ حُمِّلُوا التَّوْرَاةَ ثُمَّ لَمْ يَحْمِلُوهَا كَمَثَلِ الْحِمَارِ يَحْمِلُ أَسْفَارًا ۚ بِئْسَ مَثَلُ الْقَوْمِ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ ۚ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ﴿٥﴾
5. Mfano wa wale waliobebeshwa Tawraat, kisha wasiibebe ni kama mfano wa punda abebaye mijalada ya vitabu. Ubaya ulioje mfano wa watu waliokadhibisha Aayaat (na Ishara, Dalili) za Allaah! Na na Allaah Haongoi watu madhalimu.
قُلْ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ هَادُوا إِن زَعَمْتُمْ أَنَّكُمْ أَوْلِيَاءُ لِلَّـهِ مِن دُونِ النَّاسِ فَتَمَنَّوُا الْمَوْتَ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿٦﴾
6. Sema: Enyi Mayahudi! Mkidai kuwa nyinyi ni vipenzi vya Allaah pasina watu wengine, basi tamanini mauti, mkiwa ni wasemao kweli.
وَلَا يَتَمَنَّوْنَهُ أَبَدًا بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ ۚ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالظَّالِمِينَ﴿٧﴾
7. Na wala hawatayatamani abadani kwa sababu ya yale iliyotanguliza mikono yao, na Allaah Anawajua vyema madhalimu.
قُلْ إِنَّ الْمَوْتَ الَّذِي تَفِرُّونَ مِنْهُ فَإِنَّهُ مُلَاقِيكُمْ ۖ ثُمَّ تُرَدُّونَ إِلَىٰ عَالِمِ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٨﴾
8. Sema: Hakika hayo mauti mnayoyakimbia, hakika yatakukuteni tu! Kisha mtarudishwa kwa Mjuzi wa ghaibu na dhahiri. Atakujulisheni yale mliyokuwa mkiyatenda.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نُودِيَ لِلصَّلَاةِ مِن يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّـهِ وَذَرُوا الْبَيْعَ ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ﴿٩﴾
9. Enyi walioamini! Inaponadiwa kwa ajili ya Swalaah siku ya Ijumaa, basi kimbilieni kwenda kumdhukuru Allaah na acheni kuuza na kununua. Hivyo ni kheri kwenu zaidi mkiwa mnajua.
فَإِذَا قُضِيَتِ الصَّلَاةُ فَانتَشِرُوا فِي الْأَرْضِ وَابْتَغُوا مِن فَضْلِ اللَّـهِ وَاذْكُرُوا اللَّـهَ كَثِيرًا لَّعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ﴿١٠﴾
10. Na inapomalizika Swalaah, basi tawanyikeni katika ardhi, na tafuteni Fadhila za Allaah, na mdhukuruni Allaah kwa wingi ili mpate kufaulu.
وَإِذَا رَأَوْا تِجَارَةً أَوْ لَهْوًا انفَضُّوا إِلَيْهَا وَتَرَكُوكَ قَائِمًا ۚ قُلْ مَا عِندَ اللَّـهِ خَيْرٌ مِّنَ اللَّـهْوِ وَمِنَ التِّجَارَةِ ۚ وَاللَّـهُ خَيْرُ الرَّازِقِينَ﴿١١﴾
11. Na wanapoona tijara au pumbao wanaikimbilia na wanakuacha umesimama. Sema: Yaliyoko kwa Allaah ni bora zaidi kuliko pumbao na tijara, na Allaah Ni Mbora wa wenye kuruzuku.
Links
[1] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11569
[2] http://www.alhidaaya.com/sw/
[3] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7050&title=062%20-%20Al-Jumua%27ah