079-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Fadhila Za Swalaah Ya Jamaa'ah

 

Lu-ulu-un-Manthuwrun

 

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

 

Hadiyth Ya 79

 

Fadhila Za Swalaah Ya Jamaa’ah

 

 

 

 

عن ابنِ عمَر (رضي اللَّه عنهما) أَنَّ رسولَ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال: ((صَلاةُ الجَمَاعَةِ أَفضَلُ مِنْ صَلاةِ الفَذِّ بِسَبْعٍ وَعِشْرِينَ درَجَةً)) متفقٌ عليه

Imepokelewa kutoka kwa bin ‘Umar (رضي الله عنهما) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Swalaah ya Jamaa’ah ni bora kuliko Swalaah ya pekee kwa daraja ishirini na saba)). [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Mafunzo Na Mwongozo:

 

 

 

1. Umuhimu na amri ya kutekeleza amri ya kuswali Jamaa’ah kama vile Swalaah ya Ijumaa. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نُودِيَ لِلصَّلَاةِ مِن يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّـهِ وَذَرُوا الْبَيْعَ ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ﴿٩﴾

Enyi walioamini! Inaponadiwa kwa ajili ya Swalaah siku ya Ijumaa, kimbilieni kumdhukuru Allaah na acheni kuuza na kununua. Hivyo ni kheri kwenu mkiwa mnajua. [Al-Jumu’ah (62: 9)]

 

 

 

2. Umuhimu wake hadi kwamba katika vita inawapasa Waislamu waswali Swalaah ya jamaa’ah.

 

Rejea: An-Nisaa (4: 102).

 

 

 

3. Muislamu ana fursa za kujichumia thawabu nyingi na kubwa kwa kuswali jamaa’ah kutokana na fadhila zake zilotajwa katika Hadiyth kadhaa miongoni mwazo ni:

 

عنْ عثمانَ بنِ عفانَ رضيَ اللَّه عنهُ قالَ : سمعتُ رسولَ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يقولُ : ((مَنْ صَلَّى العِشَاءَ في جَـمَاعَةٍ، فَكَأَنَّما قامَ نِصْف اللَّيْل وَمَنْ صَلَّى الصبْح في جَمَاعَةٍ ، فَكَأَنَّما صَلَّى اللَّيْل كُلَّهُ)) رواه مسلم .

Kutoka kwa 'Uthmaan bin 'Affaan (رضي الله عنه)  kwamba: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) anasema: ((Atakayeswali Swalaah ya Ishaa katika Jamaa’ah, atakuwa kama kwamba amesimama nusu ya usiku mzima. Na atakayeswali Asubuhi katika Jamaa’ah atakuwa kama kwamba ameswali usiku wote)) [Muslim]

 

Pia:

 

 

عنْ عثمانَ بنِ عفانَ رضي اللَّه عنهُ قال : قال رسولُ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : ((مَنْ شَهِدَ العِشَاءَ في جمَاعةٍ كان لهُ قِيامُ نِصْفِ لَيْلَة ، ومَنْ صَلَّى العِشَاءَ والْفَجْر في جمَاعَةٍ، كَانَ لَهُ كَقِيَامِ لَيْلَة)) قال التِّرمذي: حديثٌ حسن صحيحٌ .

Kutoka kwa 'Uthmaan bin 'Affaan (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:  ((Atakayehudhuria Swalaah ya Ishaa katika Jamaa’ah atakuwa kama kwamba amesimama nusu usiku, na atakayeswali Ishaa na Alfajrii katika Jamaa’ah atakuwa kama kasimama usiku mzima)) [At-Tirmidhiy hadiyth hasan]

 

Pia,

 

عن أَبي هريرة رضيَ اللَّه عنهُ قال : قال رسولُ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : ((صَلاةُ الرَّجُلِ في جَماعةٍ تُضَعَّفُ عَلى صلاتِهِ في بَيْتِهِ وفي سُوقِهِ خمساً وَعِشْرينَ ضِعفًا، وذلكَ أَنَّهُ إِذا تَوَضَّأَ فَأَحْسَنَ الْوُضُوءَ ثُمَّ خَرَجَ إِلى المَسْجِدِ، لا يُخْرِجُه إِلاَّ الصَّلاةُ، لَمْ يَخْطُ خَطْوةً إِلاَّ رُفِعَتْ لَه بهَا دَرَجَةٌ، وَحُطَّتْ عَنْه بهَا خَطِيئَةٌ، فَإِذا صَلى لَمْ تَزَلِ المَلائِكَة تُصَلِّي عَلَيْهِ مَا دَامَ في مُصَلاَّه، مَا لَمْ يُحْدِثْ، تَقُولُ: اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَيْهِ، اللَّهُمَّ ارحَمْهُ. وَلا يَزَالُ في صَلاةٍ مَا انْتَظَرَ الصَّلاة))  متفقٌ عليه . وهذا لفظ البخاري

Kutoka kwa Abuu Huraryah (رضي الله عنه)  ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Swalaah ya Jamaa’ah inazidi (thawabu) na Swalaah ya mtu nyumbani kwake au dukani kwake kwa mara ishirini na tano, kwa hivyo anapotawadha akafanya vizuri wudhuu wake, kisha akatoka kwenda Msikitini, hakuna lililomtoa ila Swalaah; basi hatembei hatua moja ila hupandishwa daraja (kwa hatua hiyo), na hufutiwa dhambi kwa hiyo hatua. Atakapokuwa anaswali, Malaika wanaendelea kumswalia madamu yumo kwenye Swalaah ikiwa hatozungumza. Husema (Malaika): “Ee Allah Mswalie na Mrehemu.” Na huendelea hivyo wakati anasubiri Swalaah nyingine)) [Al-Bukhaariy na Muslim] Na hili tamshi la Al-Bukhaariy.

 

 

 

4. Bainisho la fadhila nyingi za kuswali Jamaa’ah ziloashiriwa katika Hadiyth moja kwa kauli yake Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): “Lau kama wangelijua yaliyomo humo (fadhila na faida) wangeliziendea (kuziswali) japo kwa kutambaa.”

 

Hadiyth:  

 

 

عن أَبي هُريرة رضيَ اللَّه عنهُ   قال : قال رسولُ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : ((لَيْسَ صَلاةٌ أَثْقَلَ عَلَى المُنَافِقينَ مِنْ صلاة الفَجْرِ وَالعِشاءِ وَلَوْ يَعْلَمُونَ ما فِيهما لأَتَوْهُما وَلَوْ حبْوًا)) متفق عليه .

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema: ((Hakuna Swalaah iliyo nzito kwa wanafiki kama Swalaah ya Alfajiri na ‘Ishaa. Lau kama wangelijua yaliyomo humo (fadhila na faida) wangeliziendea (kuziswali) japo kwa kutambaa)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

5. Umuhimu wake mwengine katika  Hadiyth:

 

عَنْ أَبِي الدَّرْدَاءِ، قَالَ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: ((مَا مِنْ ثَلاَثَةٍ فِي قَرْيَةٍ وَلاَ بَدْوٍ لاَ تُقَامُ فِيهِمُ الصَّلاَةُ إِلاَّ قَدِ اسْتَحْوَذَ عَلَيْهِمُ الشَّيْطَانُ فَعَلَيْكَ بِالْجَمَاعَةِ فَإِنَّمَا يَأْكُلُ الذِّئْبُ الْقَاصِيَةَ)) قَالَ السَّائِبُ يَعْنِي بِالْجَمَاعَةِ الصَّلاَةَ فِي الْجَمَاعَةِ ‏.‏ابو داود بإسناد جيد وصححه الألباني

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Ad-Dardaai  amesema: Nimesikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Hakuna mahala penye watu watatu kitongojini au jangwani ambapo hakusimamishwi Swalaah miongoni mwao, isipokuwa shaytwaan huwaghilibu. Basi shikamaneni na Jamaa’ah hakika mbwa mwitu humla mbuzi alie mbali. [aliye peke yake])). As-Saaib amesema kuhusu maana ya Jamaa’ah ni kuswali pamoja (Jamaa’ah).  [Abuu Daawuwd, isnaad yake Jayyid. Taz Swahiyh Abiy Daawuwd (547)]  

 

 

 

6. Imetajwa umuhimu wake pia katika Hadiyth ya kipofu aliyemwendea Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kumtaka ruhusa asihudhurie Swalaah kwa vile hana wa kumuongoza, lakini Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimwambia madamu anasikia Adhaan ajibu (mwito wa kwenda kuswali Jama’aah Msikitini).

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ: أَتَى النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَجُلٌ أَعْمَى فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّهُ لَيْسَ لِي قَائِدٌ يَقُودُنِي إِلَى الْمَسْجِدِ،  فَسَأَلَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ يُرَخِّصَ لَهُ فَيُصَلِّيَ فِي بَيْتِهِ، فَرَخَّصَ لَهُ فَلَمَّا وَلَّى دَعَاهُ فَقَالَ: ((هَلْ تَسْمَعُ النِّدَاءَ بِالصَّلَاةِ؟)) قَالَ: نَعَمْ، قَالَ: ((فَأَجِبْ)) رواه مسلم  

 

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba alikuja kipofu kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: Ee Rasuli wa Allaah! Hakika mimi sina mtu wa kuniongoza Msikitini. Akamuomba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amruhusu aswali nyumbani kwake. Akamruhusu. Alipogeuka, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwita na kumuuliza: ((Je, unasikia Adhaan?)) Akasema: Naam.  Akasema: ((Basi itikia)) yaani nenda kuswali. [Muslim]

 

 

7. Anayeacha kuswali Jamaa’ah amefananishwa kwa sifa za unafiki kama ilivyotangulia Hadiyth juu inayosema.

 

 

 ((Hakuna Swalaah iliyo nzito kwa wanafiki kama Swalaah ya Alfajiri na ‘Ishaa. Lau kama wangelijua yaliyomo humo [fadhila na faida] wangeliziendea [kuziswali] japo kwa kutambaa)). [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

8. Uislamu unasisitiza Waislamu kuungana kwa umoja kwa kila upande na kila hali.

 

 

Rejea: Aal-‘Imraan (3: 200), Asw-Swaff (61:4)

 

Rejea pia Hadiyth namba (20).

 

 

 

Share