Skip to main content

Mukhtasari Wa 'Aqiydah Ya Muislamu: Maswali Na Majibu47-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Nani Waliyy wa Allaah?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

47-Nani Waliyy wa Allaah? 

Waliyy wa Allaah ni Muumini mwenye taqwa mno na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).

أَلَا إِنَّ أَوْلِيَاءَ اللَّـهِ لَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ﴿٦٢﴾

Tanabahi!  Hakika vipenzi wa Allaah hawana khofu juu yao, na wala hawatohuzunika

الَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ﴿٦٣﴾

Ambao wameamini na wakawa wana taqwa. [Yuwnus: 63]

((إِنَّمَا وَلِيِّيَ اللهُ وَصَالِحُ الْمُؤْمِنِينَ)) متّفق عَلَيهِ

((Bali yeye ni kipenzi cha Allaah na Muumini mwema)) [Al-Bukhaariy, Muslim]