Wudhuu Unatenguka Akipeana Mkono Au Kugusana Na Asiye Muislamu?

Wudhuu Unatenguka Akipeana Mkono Au kugusana Na Asiye Muislamu?

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Kupeana mikono kwa kusalimiana na mtu mwanaume mwenzangu lakini si muislamu (mkristo) inatengua udhu?

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Kupeana mkono na asiyekuwa Muislamu hakutengui wudhuu kabisa kwa  si miongoni mwa mambo yenye kutengua wudhuu.

 

Huenda watu wengine wakafikiria hilo kwa kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  Ameiwaita ni najisi katika Suwrah   At-Tawbah lakini najisi walio nayo ni ule ushirikina wao wala sio unajisi kama ule unaojulikana kama wa mkojo, kinyesi na vitu vinginevyo.

 

Bonyeza viungo vifuatavyo upate faida zaidi kuhusu Twahara kwa ujumla na yanayotengua na yasiyotengua wudhuu:

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Mlango Wa Twaharaah

 

031-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Mlango Wa Twahara: Yanayotengua Wudhuu

 

032-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Mlango Wa Twahara: Mambo Yasiyotengua Wudhuu

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share